Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 29, 2013

RECHO ANAAMINI


Na Elizabeth John


MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Rachel Haule ‘Recho’, ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Niamini’ ambayo imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Recho alisema, anamshukuru Mungu nyimbo zake zinapokewa vizuri na mashabiki wake, hivyo anajitahidi kukamilisha video ya wimbo huo mwezi ujao ili kuwapa raha mashabiki wake.

“Muziki ni sehemu yangu ya kazi na sipendi mtu aidharau kazi yangu na sipendi kuwaudhi mashabiki wangu, ili kuepukana na hili nimeamua niwe natoa nyimbo ambazo zimeenda shule ili nisiwachoshe wapenzi wangu,” alisema Recho.

Recho, aliwaomba mashabiki wake wasikae mbali na yeye, kwani kuna vitu vingi amewaandalia ambavyo anaamini vitakuwa ni burudani kwao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...