Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 19, 2013

‘YAHAYA’ WA LADY JAY DEE AANZA KUTESA MTAANINa Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Joto Hasira’ mwanadada ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Yahaya’ katika vitio mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Jay Dee alisema anaomba sapoti kwa mashabiki wake na anaimani itafanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi ambayo yametumika katika wimbo huo.
“Naomba mashabiki wangu waipokee vizuri kazi hii naimani itafanya vizuri, mbali na hiyo nipo katika hatua za mwisho za uandaaji wa video ya ngoma hiyo, mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Jide.
Jide alishawahi kutamba na ngoma zake zingine kama, Natamani Kuwa malaika, Single Girl na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...