Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 19, 2013

Barclays Bank yaendesha droo ya pili ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake


Meneja Mawasiliano wa Barclays, Tunu Kavishe, (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Benki, Kitengo cha Wateja  Binafsi,  Musa Kitoi wakiwa na washindi wa droo ya pili ya Golden Briefcase Campaign jijini Dar es Salaam. 
Meneja Mawasiliano wa Barclyas, Tunu Kavishe (kulia) akiwa na washindi wa pili wa droo ya Golden Briefcase Campaign, Anorld Shirima na Khadija Kashoro.

DAR ES SALAAM, Tanzania

 Barclays Tanzania leo imefanya droo yake ya  pili ya kampeni  ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake. Droo hii inawapa fursa wateja 13 kujishindia masanduku 13 ya dhahabu kwa muda wa miezi mitatu.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa benki, kitengo cha wateja  binafsi,  Bwana Musa kitoi alisema, “ Fursa ya ushindi iko wazi kwa kila mteja (Wateja waliopo na watarajiwa) mwenye akaunti na Barclays Bank Tanzania. Leo tumekamilisha droo yetu ya pili na tumewapata washindi 13. Vile vile tunatoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza iliyofanyika tarehe 22 Mei 2013, katika masanduku kumi na tatu ya dhahabu. Kila mteja atachagua sanduku na kulifungua ili kuweza kujua zawadi yake. Zawadi zilizopo ni i-Pad, Home theatre, Mashine za kufulia na vocha za zawadi.
Bwana  Kitoi aliongeza na kusema kuwa “ukiweka pesa zako benki na ukawa na salio lililokusudiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo hii na utapata nafasi ya kujinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya tshs millioni kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa kampeni. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi tarehe11 Aprili 2013 na itaendelea hadi tarehe 30th June 2013.
Shindano hili liko wazi kwa  wateja  binafsi, wapya na wa zamani, ambao wanaweka fedha zao  na benki yetu hapa Tanzania. Wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye account ya hundi (Current Account)  au amana (Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye account kwa shillingi laki tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na salio hili libakie kwenye account hadi mwisho wa mwezi bila kupungua, Kila ongezeko la shillingi Laki tano linampatia mteja ingizo la ziada katika katika droo ya mwezi husika.
Zawadi kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000) itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays Golden Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha kuifungua ili kujua alichojishindia.  Zawadi zinazoshindaniwa kila mwezi ni  iPads 2, vocha 8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shillingi laki 2 kila mmoja (TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na home theatre 1.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...