Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 21, 2013

AMINI 'HAYUPO NAE'
Na Elizabeth John

BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Ni wewe’, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’ anajipanga kuachia video ya kibao chake cha ‘Sipo nae’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaama, Amini alisema anamshukuru mungu kazi hiyo imefanya vizuri na anaamini itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya kibao hicho.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika studio ijulikanayo kwa jina la Shany chini ya mtengenezaji mahiri Mr. T ambaye anauhakika amemtendea haki katika kazi hiyo.
“Mtayarishaji wangu namuamini sana, hivyo najua wadau wengine wataupenda wimbo kulingana na vionjo ambavyo amevitumia mbali na ujumbe uliopo katika kazi hiyo.” alisema Amini.
Pia aliwaomba wadau na mashabiki wa muziki nchini kumpa sapoti katika kazi zake na wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.  
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Amini alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Robo saa’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...