Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 16, 2010

ROGER FEDERAR ASISITIZA KUCHUKUWA UBIGWA KATIKA MASHINDANO YA WIMBLEDON


Halle, Ujerumani

ROGER Federar amesisitiza kuwa maandalizi yake ya mashindano ya Wimbledon hayajatetereka licha ya kupoteza mechi bila ya kutarajia juzi.

Mchezaji huyo nyota kutoka Uswisi ayashiriki katika Mashindano Makubwa ya England akiwa anataka kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya 17.

Lakini juzi, Federer alifungwa kwa 3-6 7-6 6-4 kwa mchezaji kutoka Australia, Lleyton Hewitt katika mashindano ya Gerry Weber Open mjini Halle, Ujerumani.

Alikwenda kwenye mechi hiyo akiwa na rekodi ya 76-1 baada ya kupoteza mechi moja dhidi ya Rafa Nadal katika fainalia ya mashindano ya Wimbledon miaka miwili iliyopita

Federer ambaye alishinda mechi zake
15za awali dhidi ya Hewitt alisema, “Ilikuwa ni bahati mbaya kutofsonga mbele lakini kupoteza hakuniogopeshi mimi.

"Ilikuwa ni mashindano mazuri kwangu. Ninatakiwa kuhakikisha ninajiandaa kwa mashindano ya Wimbledon."

Federer mwenye umri wa miaka 28, atarejea Uswisi kwa siku mbili kabla ya kuelekea London Uingereza kesho.

Hewitt mwenye umri wa miaka 29 aliye katika nafasi ya 32 kwa ubora baada ya kushinda mechi yake alisema: "Roger ni mchezaji mkubwa na kila wakati unapokwenda uwanjani kucheza naye,
Katika mechi nyingine ya maandalizi ya Wimbledon Sam Querrey alimfunga Mmarekani mwenzie, Mardy Fish kwa 7-6 7-5 katika fainali ya mashindano ya AEGON iliyochezwa Queen Club, London.

Maria Sharapova, bingwa wa 2004 wa Wimbledon alifungwa kwa 7-5 6-1 dhidi ya mchezaji kutoka China, Li Na katika fainalia ya AEGON mjini Birmingham.

Sharapova mwenye umri wa mika 23, alisema: "Li alikuwa mzuri sana dhidi yangu lakini ninatumaini kufanya vizuri Wimbledon."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...