Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 19, 2010

JE ARGENTINA NI BRAZIL WAPYA? MCHAMBUZI ANACHAMBUA NI MDAU WA BLOG HIINa alice ngubwene

Ndugu mtazamaji ukiangalia kwa makini katika kombe la dunia 2010 huwezi kukosa maneno kuhusiana na nchi za amerika ya kusini, maana hadi leo siku ya 8 leo tangu kombe la dunia tokea lianze utagundua kitu cha kushangaza kuona kana kwamba soka la argentina ndilo lililokuwa la brazil zamani

Ingawa bado ndio kwanza mashindano yanaendelea ukitizama kwa makini mechi mbili za kwanza ambazo Argentina imecheza kwa kweli utaona ni team ambayo itaonyesha nini katika kombe la dunia ila imetumia akili ya mpira wa miguu katika kutoa burudani na pia kutafuta ushindi wa kombe la dunia yaani wameonyesha nia yao wazi.

Taifa hilo likiongozwa na mwanasoka mkongwe wa dunia Diego maradona wameonyesha kandanda safi katika kushambulia na bila kuchoka na kufanya team hiyo kuwa kivutio kikubwa afrika kusini.

Ingawa ukiangalia vizuri katika mechi yao na korea ya kusini utagundu wana udhaifu kidogo kati safu yao ya ulinzi amabyo inaongozwa na Martin Demichelis ambaye alisababisha argentina kufungwa goli moja na korea ya kusini.

Wasiwasi uliotanda juu ya kipa wao ambaye ni mdogo kiumri Sergio Romero (miaka 22) anayedakia timu Az Alkmaar ya uholanzi huku agentina ikitawala michezo yote aliyocheza katika kikosi B.

Katikati ya kombe la dunia Maradona ameongoza kikosi chake amabcho kimeonyesha nia na hari ya kuondoka na ushindi huo. Ukiangalia jinsi Maradona na dunga walivyoochagua vikosi vyao , dunga yeye amechagua kikosi chake kilichosheheni viungo wazuiaji na wategemezi zaidi akijua hao hawatamwangusha katika harakati zake za kutafuta ushindi wa komeba la dunia kwa brazil kwa mara ya 6 kit ambacho maradona yeye amejaza washambuliaji zaidi katika kikosi chake.

Uchaguzi wa maradona wa wachezaji wa kushambulia sita katika kikikosi chake ambao wameshatumbukiza magoli 170 kwa miezi 12 iliyopita katika ligi zao za nyumbani , Maradona ametuma ujumbe maridhawa kabisa katika nchi zingine 31 ambazo pia zinashiriki kombe la dunia 2010 na kusema kusema kuwa haogopi kucheza mpira wa kushambulia wakati wote.

Diego maradona ni Kocha mwenye bahati kwa sababu hakuna kocha ambaye anaweza kuweka matumaini yake zaidi kati safu ya ushambuliaji ikiwa ndani yake ana mchezaji bora wa dunia Lionel Messi . Messi ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kutoonyesha ubora wake katika timu yake ya taifa , safari hii ameanza kombe la dunia kama vile anamaanisha ushindi kwa kuonyesha uchezaji wake bora katika mechi mbili.

Maradona ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa kutomfanya Messi aweze kucheza vema katika mechi za kufuzu kombe la dunia lakini bado amempa messi nafasi ya kuongoza kikosi cha argetina kama vile yeye alivyofanya mwaka 1986 wakati huo akiwa nahodha wa agentina. Uhusiano wa karibu wa wawili hao ambao unaonekana waziwazi kwa maradona kumkumbatia mara kwa mara Messi wakiwa wanaelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya filimbi ya mwsho kulia.

Pale Agentina ilipoinyuka nigeria kwa 1-0 ndipo Maradona alipoonyesha nia haswa ya yeye kutaka kumfanya messi kuwa mchezaji ambaye atakuwa karibu zaidi na mpira kwani itamletea furaha katika timu yake nzima.

Kwani inaonekana wazi kila ambapo messi anapokuwa na mpira mguuni washabiki waliofurika katika uwanja huo wa soccer city wanakuwa na shauku na pia waandhishi wote huwa makini katika kuangalia na kuona angalau messio basi anafunga goli yeye mwenyewe.

Kwa kuanza safu ya ushambuliaji Tevez anapoanza na Messi na mzamishaji mipira mitatu higuani Gonzalo na angel di maria utaona nguvu ya ushambuliaji ni ya kasi mno hsa pale mkwe wake sergio aguero alipoingia kutoka benchi la wachezaji wa akiba na kumwacha Mshmbuliaji machachari wa klabu ya intermilan

Lakini cha muhimu na kilichofurahisha zaidi ni kuwa kikosi cha maradona kimemiliki vema mpira wake katika mechi zake zote mbili za muhimu na kuweka wasiwasi katika nchi nyingine.

Wakiongozwa na mshambuliaji mwenye uchu wa magoli Tevez , wanaonekana wakifurahi jinsi wanavyomiliki mpira uwanjani. Wachezaji wa agentina wanaonekan wakifurahishwa sana na kocha wao amabye anawafanya wajisikie vema wakinwa ndani na nje ywa uwanja.
Ukiangalia kipindi cha pili katika mechi yake na korea ya kusini ambao walionyesha kuweka kasi katika kushambulia , maradona alikuwa na wakati mgumu wa kuamua kumtoa Tevez na kumuingiza Aguero ili kubalisha mfumo wa mpira upya. Na dakika mbili baadaye Higuani aliweka wazuni mpira uliokuwa umegongwa na messi katika goli, na dakika tatu baadaye tena higuain alipiga mpira kwa kichwa na kuweka golini mpira amboa alipatiwa pasi na aguero.

Maelfu ya waagentina hawakusita kuonyesha furaha yao katika kushangili ndani na nje ya uwanja wa soccer city huku wakiimba na kucheza vuvuzela kwa staili ya aina yake .

Mamia ya washabiki waliohudhuria kombe la dunia wamekuwa wakipenda kumwangalia maradona kwani amekuwando kivutio kikubwa hata anapokuwa aktika benchi lake la ufundi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...