Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 17, 2010

SASATEL YAZINDUA KOMPYUTA NDOGO


KAMPUNI ya simu za mkononi na mawasiliano Sasatel imezindua kompyuta ndogo za kuweka kumbukumbu ambazo zimeunganishwa na kifaa maalum 'Modem' kinachomuwezesha mtumiaji kuunganishwa na mtandao wa internet bila kuingia gharama za ziada .

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa bidhaa za Huduma wa Sasatel Bw.Thomas Molving alisema kompyuta hizo zimeletwa kwa lengo la kuwawezesha watanzania wenye kipato cha chini ili waweze kumiliki kompyuta na kurahisisha maisha yao kwa kutunza kumbukumbu kirahisi na kupata taarifa mbalimbali za internet.

"Tunaelewa kuwa bado ni vigumu kwa kila mtanzania kuweza kumiliki kompyuta na kuweza kujiunganishia na mtandao wa internet kutokana na gharama kubwa ndio maana tumeona tuuingize bidhaa hii sokono na kila mara tutakuwa tunajitahidi kubuni huduma zenye gharama nafuu ili kurahisisha mawasiliano ," alisema na kuongeza

Kompyuta hizi aina ya Acer Notebook zina sehemu ya kusomea taarifa yenye inchi 10.1 kumbukumbu ya GB1, sehemu ya kuhifadhi kumbukumbu na imewekwa programu ya kuzuia virusi vinavyoharibu kompyuta ambayo mtumiaji anatakiwa kuongeza nguvu kila baada ya siku 60," alisema
Alisema uzinduzi wa kompyuta hizi kwenye soko la Tanzania ni moja ya jitihada zinazofanywa na Sasatel kwani lengo lake kubwa ni kutoa huduma bora za mawasilinao , nakuwapatia wananchi huduma za kisasa za mawasiliano na kuhakikisha gharama za mawasilinao zinakuwa za bei nafuu ambazo watanzania wengi wanaweza kuzimudu.

2 comments:

  1. please email me the details of this program on jbuinda@gmail.com urgently.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...