Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 28, 2010

ZAIN WAKABIDHI ZAWADI ZA WASHIRIKI WA AFRICAN CHALENGE


Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI
Mwandishi wa habari wa chanal ten akizungumza na Justiu Rwelengera
Baadhi ya wanafunzi wakiesabu dola zao baada ya kukabidhiw kutoka kushoto ni Fredy Mwakalinga Rodriaue Sakaya Deliphinius Karumuna na Justiu Rwelengera
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu ARDHI Dr,Mbura Omari dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam, jana.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu Huria Bw. Salim Hamad, dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam, jana.Zain yakabidhi zawadi ya pesa taslim kwa Vyuo viliyoshiriki ZAC

Dar es Salaam June 28, 2010.

Zain Tanzania leo imekabidhi zawadi za pesa taslim kwa baadhi ya Vyuo Vikuu na wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya Zain Africa Challenge yaliyomalizika hivi karibuni.
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta alikabidhi Dola za Marekani 1600 kwa Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Omary Mbula pamoja na Salim Hamadi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam kwa ushiriki wa vyuo vyao katika mashindano ya ZAC. Dola 1000 ni za chuo wakati dola 600 ni kwa ajili ya washiriki sita kutoka vyuo hivyo ambapo kila mwanafunzi, kocha na mratibu wanapata dola 100 kila mmjoja
Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi kila mmoja jana alipata dola za Marekani 500. Chuo Kikuu cha Ardhi ni miongoni mwa Vyuo Vikuu vitano vilivyofuzu kuingia fainali nchini Uganda. Chuo cha Ardhi pia kitapewa dola za Marekani 5000 za kukisaidia chuo na pesa hizo zitaingizwa katika akaunti ya chuo kuboresha elimu chuoni hapo..
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania alitaja Vyuo Vikuu vingine vitakavyopokea pesa za ZAC kama; Chuo Kikuu cha Sokoine University na Chuo Kikuu cha Mzumbe kutoka Morogoro, Saint John na Chuko Kikuu cha Dodoma kutoka Dodoma, pamoja na Teofilo Kisanji University kutoka Mbeya na State University cha Zanzibar. Vyuo hivi kila kimoja kitapata dola za Marekani 1000 fedha za chuo na kila mshiriki kati ya washiriki sita atapata dola.
Aidha alivitaja vyuo vitakavyopokea Dola za Marekani 10,000 kama fedha za chuo na kila mshiriki kuondoka na dola 1000 kuwa ni chuo kikuu cha Arusha University na Chuo Kikuu cha Tumaini ambavyo vilifuzo kuingia fainali zilizorushwa kwenye luninga. Chuo kikuu cha Zanzibar kwa upande wake kitapata dola za Marekani 5000 na kila mshiriki dola 500. Chuo hiki ni miongoni mwa vyuo vikuu vitano vilivyofuzu kushiriki katika mashindano ya Kampala.
Zain iliwekeza zaidi ya dola za Marekani 1000,0000 katika Zain Africa Challenge mwaka huu ikiwa ni sehemu ya programu yake inayolenga kukuza elimu barani Afrika

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...