Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 23, 2010

KLABU MAISHA KUANZA KAZI KESHO

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa klabu ya Maisha ambayo ilikuwa imeteketea kwa moto miezi michache iliyopita na leo itaanza maonesho yake rasmi baada ya kusimama kwa mda

KLABU ya Usiku ya Maisha inatarajiwa kufunguliwa tena hii Kesho kuendelea na shughuli zake za burudan baada ya kufanyiwa marekebisho upya tangu kuungua kwake.

Maisha Club iliyokuwa ikiendesha burudan nyakati za usiku uliungua kufuatia ajali ya moto na kufanyiwa marekebisho tena kuanzia Januari 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Dj Majay) alisema ukumbi huo kwa sasa umeboreshwa zaidi tofauti na awali kutokana na kuweka mbele tahadhari kwa ajili ya usalama wa wateja wao.

Alisema maboresho hayo yametokana na kuangalia hasara kubwa ambazo zinaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kudhuru afya za wateja wao na matatizo mengi na kuamua kuingia gharama zaidi katika ujenzi na maboresho.

"Baada ya kuangali juu ya ajali ile ya moto, tukaona kuwa kuna mambo mengi ambayo yalikosewa kitu kilichofanya kuanza upya ujenzi wa kisasa wa jengo maalum la shughuli za buruda nyakati za usiku (Night Club) ambayo itakuwa na hadhi ya kimataifa.

"Hilo likatufanya kuingia gharama zote ambazo kwa sasa zinafanya ukumbi huu kuwa wa kisasa zaidi na kama unavyoweza kuwa wa kisasa ukilinganisha na nyingine kubwa ndani na nje ya Tanzania," alisema mkurugenzi huyo.

Jengo hilo la sasa lenye vitu mbalimbali vilivyoongezwa kama luninga zilizounganishwa na channel za kimataifa za burudani, sehermu maalum za kuvuti sigara, vyumba saba vya kuuzia vinywaji, imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 2.2 mpaka sasa inapokamilika.


Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey),akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi rasmi wa Club Maisha,shoto ni Meneja wa Club hiyo Allan Ngugi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...