Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 21, 2010

TAMASHA LA MTEMI MIRAMBO KUFANYIKA TABORA MWEZI UJAO


Wahandishi wa habari Dina Ismahil na Cecilia Jeremia walikuwepo kupata habari kamili
Meneja wa bia ya Balimi (TBL) Fimbo Butallah (kulia) na Mkurugenzi wa Chief Promoshens. Amon Mkoga wakiwaonesha waandishi wa habari picha mbalimbali za utamaduni Tabora wakati wa mkutano wa kutambulisha tamasha la Mtemi Mirambo Dar es salaam jana litakalofanyika mwezi ujao mkoani TaboraChief Promotions imeandaa Tamasha la Ngoma za utamaduni liitwalo MTEMI MIRAMBO,lenye lengo la kukuza sanaa na kuvitangaza vikundi vya ngoma vilivyopo katika mkoa wa Tabora.
Tamasha hilo litaanza kufanyika katika viwanja vya chipukizi Tabora kuanzia Tarehe 16 - 18 Julai,2010 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
Siku hiyo shughuli mbali mbali zitafanyika kama vile maonyesho ya ngoma za asili,Sarakasi,Ngonjera na Nyakula vya asili.mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Moshi Mussa Chang'a.
Tamasha hili linakuja kwa udhamini mkubwa toka kwa kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi,Bodi ya Utalii (TTB),Zain Tanzania na Merina Investment.
Chief Promotions imesajiliwa mwaka 2003 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Baadae Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,na imefanya kazi na Mashirika mengi tu yakiwemo ya Umoja wa Matiaifa (UNAIDS,WHO,UNDP) na pia imefanya kazi na TBL,NSSF,TACAIDS na mengine mengi.
kwa mawasiliano
Amos Mkonga,

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...