Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 27, 2010

MCHEZA GOFU SAYORE AIBUKA NA BLACKBERR KUTOKA ZAINGidion Sayore akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya gofu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam. Sayore aliibuka mshindi wa jumla na kuzawadiwa simu ya mkononi aina ya Blacberry.

Gofu yamzawadia Blackberry Sayore

Na Mwandishi wetu

Gidion Sayore amejinykulia simu ya kisasa ya mkononi aina ya Blackberry baada ya kuibuka katika mashindano ya gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Sayore ambaye ni mchezaji mkongwe katika mchezo wa gofu aliibuka mshindi katika mashindano hayo baada ya kupata pointi 31 na kumzidi mpinzani wake Simon Sayore ambaye ni mdogo wale aliyepata point 29.

Sayore ambaye ni mmoja wa wachezaji wa gofu kwa upande wa wazee katika klabu ya gofu ya Lugalo aliwashukuru wadhamini wa mchezo huo na kutoa wito kwa makampuni mengine yajitokeza kuinua mchezo wa gofu Tanzania.

“Nayaomba makampuni mengine yaige mfano wa Zain kwa kuinua mchezo huu apa nchini kwetu mchezo wa gofu ni mchezo mzuri kama unavyoona michezo mingine ni vizuri kama makampuni mengine yataona umuhimu wa mchezo huu na kuufanya uwe kama michezo mingine.,” alisema Sayore.

Mashindano hayo ambayo ushirikisha wachezaji wa rika mbalimbali yamekuwa yakifanyika kila mwisho wa wiki chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya mkononi ya Zain Tanzania.

Washindi wengine ni Priscus Nyoni , Joseph Evans, Stephania Sayore. Wasindi hao wote walijipatia zawadi mbalimbali zikiwemo seti za vyombo vya ndani na miamvuli.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...