Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 17, 2010

SNOOP DOG KUTUMBUIZA UINGEREZA


Snoop Dogg kutumbuiza kwenye tamasha Uingereza

LONDON, Uingereza

SNOOP Dogg ataungana na wanamuziki wengine katika tamasha ambalo litafanyika Uingereza wiki ijayo.

Miongoni mwa wasanii atakaungana nao ni Muse, Gorillaz na Stevie Wonder.

Alisema: "Niko katika tamasha hilo kwa kushinda na itakuwa kama matairi manne yaliyolala, umeshanisikia mimi UK?"

Mwanamuziki huyo haamini kung'ara kwa hip-hop, katika tamasha lakini anaamini atafanya vizuri kwenye tamasha la Glasto.

Alisema: "Kila wakati ninapokuwa UK ninaripuka. Ninaangalia mbele kwenda pale."

Mwanamuziki huyo ni rafiki wa mwanasoka mahiri wa England, David Beckham au "D Becks" kama Snoop anavyomwita, hatakuwa katika tamasha hilo kwa kuwa yuko kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Afrika Kusini.

Katika fainali hizo zinazoendelea, Snoop amekuwa mshabiki wa Brazil, pamoja na kwamba Marekani iko katika fainali hizo.

Snoop atafanya ziara na kufanya onesho katika Uwanja wa O2 mjini Glasgow Julai 4, mwaka huu na kisha mjini London kwenye Uwanja wa O2 Bush Empire Julai 9, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...