Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 24, 2010

England NA Ghana ZAINGIA 16 BORAWachezaji England wakishangilia baada ya kufunga goli
England, Marekani zapeta 16 Bora

Maumivu yaendelea kwa timu za Afrika

PORT ELIZABETH, South Africa

HATIMAYE timu za England na Marekani, jana zilikata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Dunia, yanayofanyika nchini Afrika Kusini kwa kila moja kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya wapinzani wao.

Kwa matokeo hayo timu hizo, zilifanikiwa kutuliza mzuka za mashabiki wao, ambao walikuwa hawana raha kutokana na kuanza vibaya michuano hiyo, inayofanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika

Ikicheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi England ikiwa Kundi C, ilipata goli lake pekee kupitia kwa mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe, dhidi ya Slovenia ambayo nayo ilikuwa ikipambana ili kupata ushindi.

Defoe ambaye alicheza kuanzia mwazo, aliunganisha mpira wa krosi kutoka kwa James Milner katika dakika ya 23 na kuifanya Englad, kupata ponti tatu na kufikisha tano na kuwa kinara wa kundi hilo

katrika mechi ilichezwa mjini Pretoria.

Slovenia iliyokuwa kinara wa kundi C, ikiwa na pointi nne imejikuta kitumbua chake kikiingia mchanga kutokana na Marekani nayo kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Algeria iliyokuwa na pointi moja na kuchumpa hadi nafasi ya pili hivyo yenyewe kuachwa nje.

England ilicheza mechi hiyo kwa umakini, huku ikizuia kufungwa na huku ikishambulia toka mwanzo.

Bao la Marekani iliyokuwa ikicheza katika Uwanja wa Loftus lilifungwa na Landon Donovan, ambaye alimpiga chenga kipa wa algeria, Rais Bolhi katika dakika za majeruhi, baada ya kutema shuti la Clint Dempsey.

Hilo lilikuwa ni goli la nne kwa Donovan katika fainali hizo za Kombe la Dunia, akiwa sawa na Bert Patenaude wa Marekani pia.

England sasa katika hatua ya mtoano itacheza na mshindi wa pili kutoka kund D, lenye timu za Australia, Serbia, Ghana na Ujerumani. Wakati Marekani itacheza na mshindi wa kwanza wa Kundi D.

Leo katika mfululizo wa mashindano hayo Kundi F: Paraguay itachuana na New Zealand na Slovakia itacheza na mabingwa watetezi Italia saa 11 jioni.

Usiku saa 3:00, Cameroon itachuana na Uholanzi na Ghana itacheza na ujerumani. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...