Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 16, 2010

MICHAEL BALLACK KUSAIN MAN UNITED


LONDON,Uingereza

KOCHA wa Man United ameingia katika mbio za kutaka kumsaini kiungo Michael Ballack ambaye ameachwa na timu yake ya Chelsea.

Kocha huyo wa Manchester United amepanga kumpati ofa ya mkataba wa mwaka mmoja nahodha huyo wa Ujerumani ambaye ni majeruhi ili achezea Old Trafford huku akiwa na uamuzi wa kuongeza mkataba wa miezi mingine 12, kwa mujibu wa taarifa.

Kumekuwa na taarifa kuwa wamiliki wa kimarekani wanadaiwa deni linalokaribia pauni bilioni moja, kunaweza kusiwepo fedha za kumsaidia

Ferguson kusaini katika majira haya ya joto, Kocha huyo tayari amemnyakua Javier Hernandez mchezaji Javier Hernandez kwa ada ya pauni milioni 7.5.

Ballack, hajawahi kufikiria kuchezea United wala kuwa shabiki wa timu hiyo katika kipindi kilichopita, anatakiwa na klabu kubwa Ulaya ya
Real Madrid na Tottenham nayo inasemekana kumhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

Klabu yake ya zamani Bayer Leverkusen nayo inamhitaji lakini inaweza isimudu kiwango chake cha mshahara kama alichokuwa akipata Chelsea.

Ballack amekosa kucheza fainali za Kombe la Dunia kutokana na kuumia enka, klabu ya Werder Bremen nayo imegwaya kumpata kwa kigezo cha mshahara ambapo inaelezwa kuwa hata kocha wa Wolfsburg,Steve McClaren naye anamtamani.

Ballack amekosa kucheza fainali za za Kombe la Dunia baada ya kuumia katika mechi ya fainali ya kombe la FA wakati akichezea Chelsea ilipokuwa ikichuana na Portsmouth na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ballack alifunga magoli manne katika mechi 38 msimu uliopita, pia alikuwa ni mmoja wachezaji waliosaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Engand, ameacha na timu hiyo baada ya kupewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...