Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 24, 2010

SIMBA YAPATA KATIBU WA KUAJIRIWA MPYA


Simba SC yapata mrithi wa kaduguda

Na Shaban Mbegu

UONGOZI wa Simba, umetangaza jana ilimtangaza Katibu Mkuu mpya wa kuajiriwa, Evadus Mtawala ambaye atakuwa akifanya kazi zote za utawala za Klabu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Aden Rage alisema Mtawala amepewa kazi hiyo baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhika naye.

Alisema licha ya Mtawala kupewa jukumu hilo Kamati ya Utendaji pia ilimtangaza Deoniz Malinzi kuwa mlezi wa Klabu baada ya kuridhika na sifa alizonazo.

Rage alisema Kamati hiyo pia iliwatangaza wadhamini wa Klabu hiyo kuwa Ramesh Patel, Hamisi Kilomoni, Mzee Abdulahib na Abbas Sykes ambaye amekuwa mdhamini tangu Klabu hiyo ilipoanzishwa.


Akizungumzia wasifu wa Mtawala, Rage alisema kitaaluma ni mwanasheria na pia ni mtaalamu wa mambo ya komputa, lugha za Kifaransa, Kiswahili na Kiingereza.

"Huyu ndiye tunatarajia atakuwa ni Katibu wetu wa kuajiriwa, lakini kwa sasa tumempa muda wa miezi mitatu kuangalia utendaji wake, kama tutaridhika nao tutampa jukumu hilo moja kwa moja", alisema.

Katika hatua nyingine Rage ameliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kutoa ufafanuzi juu ya sheria mpya ambayo waitangaza kuhusiana na kusajili wachezaji watano wa kigeni, badala ya kumi kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Alisema kutokana Simba kukabiliwa na mashindano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu ndiyo maana wanahitaji kuwa na wachezaji wengi wa kigeni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.

Wakati huo huo Rage jana alitangaza rasmi kuwania Ubunge wa jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu ujao unatarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...