Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 15, 2010

BWAGAMOYO SOUND KUTUMBUIZA SAADAN CLUB BAGAMOYO JUMAMOSI


Mwinjuma Muumin ‘Kocha wa Dunia’ akiwa katika moja ya kazi alizopata kufanya wakati akiwa na bendi tofauti tofauti
Na Edgar Nazar, Bagamoyo

BENDI ya muziki wa dansi ya Bwagamoyo Sound International ‘Gusa unase’ iliyo chini ya Mwinjuma Muumin ‘Kocha wa Dunia’ inatarajiwa kufanya onyesho kubwa mjini Bagamoyo jumamosi ya wiki hii pamoja na bendi mpya ya Chikicha Original iliyochini ya Masoud Kilimanjaro katika ukumbi wa Saadan Club mjini hapa.

Akizungumzia onyesho hilo, Juma Mbizo ambaye ni mratibu wa onyesho hilo amesema kuwa wakazi wa Bagamoyo watarajie kupata burudania ya uhakika kutoka katika bendi hizo amabzo abdo mpya kwa wakzi wa Bagamoyo na wa vitongoji vyake.

“Sasa wakati wa kuburudika kwa wakazi wa Bagamoyo umefika ambapo watarajie kuburudika kutoka kwa kaka yao Muumin ambaye sasa anakuja na vitu vipya vikali ambavyo sasa vinatikisha katika ulimwengu wa muziki wa dansi” ameasema Mbizo.

Amesema kuwa hivyo wakzi wa Bagamoyo na wa vitongoji vyake wajitokeze kwa wingi siku hiyo ya Jumamosi ili kuja kuona mambo mapya ambapo Muumin amesema atashusha burudani ambayo itakuwa haiwahi kutolewa na bendi yeyote hapo Bagamoyo.

Mzee Mbizo ameongeza kuwa pia kwa wapenzi wa Chikicha kipenzi chao MAsoud Kilimanjaro naye atashusha ammbo mpya yakinogeshwa na wacheza shoo wa ukweli ambao wataburudisha kushinda sijku ambayo waliitambulisha bendo hiyop ambayo maskani yake yatakuwa mjini hapa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...