Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 16, 2010

OSCAR de la HOYA KUPAMBANA KATI YA FLOYD MAYWEATHER AU MANNY PACQIAO


Floyd Mayweather OSCAR de la Hoya
LAS VEGAS, Marekani
OSCAR de la Hoya amesema kuwa mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wanakaribia kukubaliana kuhusu malipo ya pambano kati yao ambalo linasumbiriwa kwa hamu.

Awali ilikuwa ikihofiwa kuwa wawili hao hawataweza kupigana kutokana na kutoelewana kuhusu kufanyika kwa kupimo cha damu kitu ambacho kilisababisha kutofanyika kwa pambano lao Machi mwaka huu.

Awalia Mayweather aliweka shari mpinznai kwa kupimwa damu mara kwa mara kabla ya pambano lama ilivyo katika mashindano ya Olimpiki kitu ambachi kilipingwa na kambi ya Pacquiao ikidai kuwa ni udhalilishaji.

Lakini mkuu wa kampuni ya Golden Boy, De La Hoya amesema kwua kambi zote mbili zinajiandaa kmusaini mkataba.

Alisema: "Siwezi kuzungumza kwa sasa kwandani kuhusu makubaliano lakini ninaweza kukuhakikishia kuwa wanakaribia sana.

"Hadi sasa, huko nyuma ilikuwa ngumu katika kukubaliana kwa sababu nyingi lakini lakini sasa sasa inakaribia.

"Ninafikiri kuwa kwa sasa tunakarinia sana kumalizia mikataba.

"Itakuwa ni pambano kubwa, pambano Kubwa!”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...