Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 17, 2010

Mohamed Mtambo kumvaa Abuu Jumaa kwa TIKETI YA CCM KATA YA JANGWANI


AKIWA KATIKA PICHA YAKE YA POZI
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO
MFANYABIASHARA Bw.Mohamed Mtambo ametangaza nia ya kugombea Udiwani wa kata ya Jangwani kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kwasasa nafasi hiyo inashikiliwa na Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Bw.Abuu Jumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Bw.Mtambo alisema ametangaza nia hiyo ili kusaidiana na wananchi wakata hiyo katika shughuli za kuleta maendeleo.

Bw.Mtambo alisema katika kulifanikisha hilo tayari ameshaanzisha shirika lisilo la kiserikali liitwalo 'World Youths Development empowerment network' litakalosaidia kuleta maendeleo ya vijana kwa kuwaendeleza kielimu na kuwatafutia shughuli mbalimbali za kufanya.

"Niayamgu kuwania nafasi hii ni kuleta maendeleo kwa wananchi wa Janwani kupitia NGO hii niliyoianzisha,hasa kwa kuwainua vijana ambao baadhi yao wapo mitaani wakiwa hawana kazi nawengine kutojiendeleza kwakukosa fedha"alisema Bw.Mtambo.

Bw.Mtambo alisema kupitia shirika hilo anampango wa kuanzisha mfuko wa kata utakaokuwa na lengola kuwakopesha fedha wazazi wa kata hiyo wasionauwezo ili kuwasomesha watoto wao na kisha kuzirudisha bila riba.

Katika hatua nyingine alisema kuwa atahakikisha viwanja vya wazi vilivyotengwa kwa michezo haviuzwi kama inavyofanywa na baadhi ya watendaji nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...