Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 12, 2010

COCA COLA YAGAWA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA


Meneja Masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza, Vida Nasari (kulia) akimkabidhi mfano wa tiketi mshindi wa promosheni ya 'Kwea Pipa na Coca Cola', Sarah Samwel Dar es Salaam jana, katikati ni Meneja wa Biashara wa Kampuni hiyo, Stephen Akyoo.(Picha na Zuberi Mussa)

68 wakabidhiwa tiketi za Kombe la Dunia

Na Zahoro Mlanzi

KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, jana imekabidhi mfano wa tiketi kwa za washindi 68 wa Kombe la Dunia, pamoja na kuzindua televisheni maalumu kwa ajili ya kuzishuhudia fainali hizo zilizoanza jana Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Vida Nasari alisema promosheni hiyo ilianza Machi 31, na ilifikia tamati Mei 31, mwaka huu ambapo jana walihitimisha shughuli hiyo kwa kutoa orodha ya Watanzania walioshinda tiketi hizo.

Alisema washindi hao pamoja na wengine kutoka Bonite Bottles na Nyanza Bottles, wataungana katika safari ya kwenda kushuhudia mechi kati ya Brazil na Ureno, itakayopigwa Juni 25, mwaka huu mjini Pretoria.

''Mbali na kukabidhi tiketi hizo, pia tunatoa zawadi kwa washindi saba wa televisheni bapa aina ya Sony, nina imani wataanza kuzitumia katika fainali hizo za Kombe la Dunia,'' alisema Nasari.

Alisema taratibu zote za safari ya washindi hao zipo katika hatua ya mwisho, ili kuwawezesha kwenda Afrika Kusini kwa kuhakikisha wanalipia hati zote za kusafiria, kwani kupeleka Watanzania 200, katika fainali za michuano hii ni tukio la kihistoria.

Baadhi ya washindi waliokabidhiwa mfano wa tiketi hizo ni Sara Pima, Hamed Said, Leonard Makungu, Joseph Mkandinyile, Boniventure Mosha, Astery Mushi, Joseph Shogholo na Salum Muhene.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...