Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 12, 2010

PWANI WAMFURAIA MINZIRO

Pwani wafurahia Minziro kuifunza Ruvu Shooting

Na Omary Mngindo, Kibaha

UJIO wa kocha Fred Felix Minziro, kuja kuifunza kwa mara nyingine timu ya Ruvu Shooting iliyopanda Kuu ya Vodacom umepokelewa kwa furaha na wadau wa soka mjini hapa.

Wakizungumza mjini hapa juzi wadau hao Msafiri Sanjito, John Pilla na Haroun Bhindo walisema ujio wa kocha huyo ni faraja kwani ana kila sifa ya kukinoa kikosi hicho.

Walisema mara baada ya kusikia uongozi wa Ruvu kuwa umeingia mkataba na kocha huyo, wadau hao walijawa na furaha kutokana na uwezo wa kocha huyo ambaye amewahi kuzinoa timu mbalimbali za Ligi Kuu ikiwemo JKT Ruvu.

"Tunaupongeza uongozi wa kambi ya Ruvu kwa kuona umuhimu wa Minziro, ambaye amejizolea sifa katika kazi yake kwa kuzinoa timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu," alisema Pilla.

Pilla alisema Minziro ana mbinu za ligi hiyo, hivyo kujiunga na Ruvu Shooting kumeonesha mwanga mpya kwa timu hiyo ambayo ipo chini ya Kanali Menas Mbele.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...