Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 12, 2015

NGUMI ZA VUNJA JUNGU KUPIGWA BAGAMOYO JUMAPILI UKUMBI WA TASUBADVD ZA SUPER D BOXING COACH ZILIZOPO SOKONI
Na Mwandishi Wetu
 Bondia Shabani Kaoneka sasa atapanda ulingoni juni 14 jumapili hii kukabiliana na Cosmas Kibuga  uzito wa kg 72 baada ya mpinzani wake wa mwanzo Said Mbelwa kuingia mitini akizungumzia mpambano uho mwandaji Muhsin Shaliff amesema kuwa maandalizi ya mpambano uho yamekamilika kwa asilimia 98 kufikia 100

mbali na mpambano uho wenye upinzani mkali kutakuwa na michezo mingine itakayo wakutanisha Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume wa Manzese mpambano wa kg 61 mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini

siku hiyo pia kutakuwa na bondia Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' atakaepambana na Mrisho Rajabu 'Dame' wakati bondia kutoka Kiwangwa Bagamoyo Iddi Pialali 'Simba aliyejeruiwa' atakumbana na Sweet Kalulu mpambano wa kg 63 raund sita

ngumi zingine zitawakutanisha Raymond Mbwago atapambana na Halidi Honga

siku hiyo pia kutapambwa nja burudani kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...