Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 7, 2013

WAREMBO WA REDDS MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI




Mikumi mkoani Morogoro, Lidya Mandara akiwaPA MAELEZO warembo wa Redds Miss Tanzania 2013 juu ya bwawa la viboko na mamba lililopo katika hifadhi hiyo wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 
Afisa Msadizi wa uhamasishaji Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Lidya Mandara akiwapa maelezo warembo wa Redds Miss Tanzania 2013 juu ya bwawa la viboko na mamba lililopo katika hifadhi hiyo wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. 
Warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya taifa Mikumi jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiruka kwa furaha mara baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa Mikumi wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini. (Picha na Intellectuals Communications Limted)

MSAMA; WAUZAJI WA CD FEKI KUSAKWA KILA KONA



  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watu 20 wanaojihusisha na uuzaji wa CD Feki za kazi za wasanii. (Picha na Francis Dande) 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akionesha ‘CD Feki’ za wasanii mbalimbali zilizokamatwa katika operesheni maalumu ya ‘safisha CD feki kila kona’ ambapo wafanyabiashara 20 katika maeneo ya Kimara, Ubungo na Manzese jijini Dar es Salaam, zikiwa na thamani ya sh. milioni 18. 
 Hivi ni vifaa vinavyotumika katika kudurufu kazi za wasanii.
 Moja ya kompyuta zinazotumika katika kudurufu kazi za wasanii.
Baadhi ya CD Feki zilizokamatwa katika Operesheni ya Safisha CD Feki.

Friday, September 6, 2013

KALIZA WA TRA DODOMA AFAGILIA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza katikati akiwa na promota na mdau wa masumbwi Mohamedi Bawazir kushoto Bondia Fransic Cheka na Fransic Miyeyusho wakati walipokwenda Dodoma kutembelea bunge la jamuhuri ya muhungano wa Tanzania baada ya Cheka kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBF na kualikwa chakula cha jioni na meneja huyo mjini Dodoma  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia  wakiwa katika picha ya pamoja na  Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza  na kuarikwa kwa chakula cha jioni na meneja huyo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya wadau wa masumbwi na mabondia wakigongesheana grass na Meneja wa Tanzania Revenue Authorithority 'TRA' Mkoa wa Dodoma Bw. Thadeo Kaliza wakati wa kutakiana heri baada ya wadau hawo wa masumbwi kupewa heshima ya kutembelea bungeni kwa mara ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI ZANTEL IKULU DAR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Simu za mkononi Zantel, Pratap Ghose, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,  akiwa na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zante, waliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

RAIS KAGAME USO KWA USO NA RAIS KIKWETE


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.(picha na Freddy Maro)

KINANA, NAPE KUUNGURUMA SHINYANGA, SIMIYU, MARA




Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maandalizi ya zira ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

NA MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana, wiki ijayo ataanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi Nape Nnauye, alisema, ziara hiyo ambayo naye atakuwemo, itaanzia katika mkoa wa Shinyanga Septemba 10 hadi 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 hadi 19, pia kwa kutembelea wilaya zote tano.

Nape alisema, Kinana atahitimisha ziara hiyo katika mkoa wa Mara ambako atatembelea katika wilaya sita za mkoa huo kuanzia Septemba 20 hadi 25, mwaka huu.

Alisema pamoja na kuwa ziara hiyo ya kikazi ni ya kawaida, lakini lengo kuu ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama, kukagua na kuimarisha uhai wa chama na  kuhamasisha wananchi wa maeneo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya wafugaji, kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha yao na ya taifa kwa ujumla.

"Katika ziara hiyo Katibu Mkuu, takagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara", alisema Nape.

Alisema, pia katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.

Thursday, September 5, 2013

MOHAMED BAWAZIRI AKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA KUHAMASISHA NGUMI NCHINI


Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na  promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na 
Catherini Matili  Picha www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na  promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


PROFESA MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI PAMOJA NA PROMOTA MOHAMEDI BAWAZIRI

CHEKA ATINGA BUNGENI NA UBINGWA WA WBF



Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI
Mbunge Wa Same Mashariki, Anne Kilango  katikati akiwa  na bingwa wa unia wa wbf fransic Cheka kulia kwake na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia na wadau wengine wa mchezo wa masumbwi nchini walipotembelea Bunge la Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakiongozwa na Mohamed Bawazir Katikati wakiwa katika picha ya pamoja kabla awajaingia ndani ya bunge kusikiliza bunge la Tanzani Super d Wa nne kulia nae akiungana nao pamoja
Bondia fransic Cheka akiwa na wabunge mbalimbali pamoja na mwanaseria mkuu wa Selikari le alipotembelea bungeni

Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt,Fenela Mukangala wa pili kushoto akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdala pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na 
Catherini Matili  Picha www.superdboxingcoach.blogspot.com

Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa na mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Fransic Cheka wakati walipo tembelea bungeni Dodoma kwa ajili ya kutambua mchango wao na kuwapongeza picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

CHEKA ATINGA NA UBINGWA WA WBF BUNGENI


Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, September 3, 2013

MIYEYUSHO VS MOMBA SASA KUPAMBANA SEPTEMBER 29 MANZESE


Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishiana misuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika September 29 katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


NA MWANDISHI WETU
MABONDIA Fransic Miyeyusho na Sadiki Momba wametambulisha mpambano wao wa kirafiki wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam

Akizungumza mmoja wa waratibu wa mpambano huo Ramadhanu Uhadi 'Rama Jah' amesema mpambano huo uliokuwa ukisubiliwa na mamia ya mashabiki wengi baada ya mabondia howo kutambiana kwa mda mrefu bila ya kuwepo na mpambano wao

ameongeza kwa kusema siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi likiwemo ya vijana chpkizi na wakongwe vile vile watakuwepo
baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo katika utangulizi ni 

Mussa Sunga atakaemenyana na Fadhili Awadhi  raundi 6 uku bondia Iddy Mnyeke kotoka kambi ya Ilala akimenyana na Keis Amari  mpambano wa raundi 4 na Ambukile Chusa atapambana na Fadhili Kambi 

Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin


--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

TASWIRA ZA WAFANYAKAZI WA STRABAG WAJENZI WA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DAR ES SALAAM (DART ) WAFUNGIWA NJE NA UONGOZI


 Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), ya Strabag, wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia makao makuu ya kampuni hiyo, Ubungo, Dar es Salaam asubuhi hii baada ya uongozi wa kampuni hiyo kuwafungia nje, kutokana na mgomo wa kudai maslahi zaidi kufanyika jana.

Kwa Picha Zaidi Na Chanzo BOFYA HAPA

Tutaitaka nafasi ya pili kwa Gambia-Kim


Kocha Kim Poulsen
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wanaipa umuhimu mkubwa mechi ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia kwa lengo ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wa pili katika kundi hilo.
Mechi hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho (Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Dakar, Senegal.
Kim amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa wameshatolewa lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango (rankings) vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka kuanzia ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa fainali za 2015.
“Tunacheza mechi hii tukiwa katika mazingira magumu, kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na hali hii tangu nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Kim.
Amesema kwa mipango ya timu yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi wanavyofikiria, na uamuzi wake wa kumwita beki Henry Joseph amezingatia mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi anayocheza na uzoefu wa mchezaji aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu ya Kongsvinger IL.
Wachezaji majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John Bocco.
Vilevile wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuwemo kwenye safari baada ya klabu yao ya TP Mazembe kutuma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wagonjwa.
Wachezaji wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.

MPAMBANO WA floyd mayweather vs canelo alvarez WAPAMBA MOTO NI WIKI IJAYO SEPTEMBER 14 MGM GRAND




floyd mayweather Kushoto na   canelo alvarez


WASANII WA BONGO MOVIE WAIPONGEZA KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS KWA UZINDUZI WA FILAMU YA LULU IITWAYO FOOLISH AGE NA KULETA USHINDANI


Uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ambayo waigizaji wakuu ni Elizabeth Michael(Lulu), Diana Kimaro, Ombeni Phir, Jengua na Hashim Kambi ulifanyika wikiend iliyopita Mlimani City, Dar es salaam, na kuwa na mafanikio kwa watu na mastaa wa filamu kuhudhuria vizuri. Mastaa kadhaa walizungumza na Swahiliworldplanet na kutoa maoni yao juu ya uzinduzi huo na kampuni ya Proin Promotions kwa ujumla iliyofanikisha uzinduzi huo ambayo pia ni kampuni mpya inayojihusisha na usambazaji wa filamu Swahiliwood. Maoni ya baadhi ya mastaa wa filamu kuhusu uzinduzi huo ni haya hapa chini.............

Shamsa Ford: Kwa upande wangu kila kitu kilikuwa sawa, pia ni faraja kwetu wasanii kuona wasambazaji wanaongezeka.

Slim Omar: Kwa upande wangu nimejifunza kwasababu ni kitu kipya na kama mapungufu basi ni kawaida katika jambo lolote, lakini kwa kweli ni mwanzo mzuri sana na wa kujifunza kwa wasambazaji na wadau wote wa filamu Tanzania, nawapongeza sana waliofanikisha ni jambo zuri na la kuigwa.

Nice Mohamed(Mtunisy): Sikuwepo hivyo ni ngumu kutoa maoni.

Efranciah Mangii: Uzinduzi ni mzuri na umefana tunachohitaji ni mafanikio kwa sisi wasanii kutokana na kazi zetu tunazozifanya, kampuni za usambazaji zipo japo hazitoshi wasanii tunaongezeka daily kutokana na hilo wasambazaji wamekuwa wakiwalipa wasanii pesa kidogo zisizokizi mahitaji ya msanii kwa Proin Promotions wamefanya kitu kizuri iwe mfano kwa kampuni nyingine za usambazaji ili kujua thamani ya msanii na kazi zake.

Yobnesh Yusuph(Batuli): Kwanza nampongeza sana Lulu, unapokuwa kioo cha jamii watu wengi wanakuangalia aidha kwa ubaya au kwa uzuri na kwa mapito aliyopitia Lulu kila mtu alitegemea hakuna jipya tena kutoka kwake lakini imekuwa sivyo alinyoosha mikono yake juu na mungu ni mwema akatenda miujiza kwake. Nampongeza sana kwa jitihada zake, namuomba awe mpya kabisa kampuni ya Proin imemfanyia uzinduzi wa heshima na hadhi kubwa. Lulu ajitambue na akubali kuwa amekuwa sasa sio mtoto tena, aonyeshe makubwa zaidi na ajilinde na scandals zisizo na lazima, achague pa kwenda hasa kwa weekend na aangalie  kampani alizonazo. Shule ni muhimu na azidishe taaluma yake, atambue ana marafiki na maadui pia namtakia kila la kheri.

Nawapongeza Proin Promotions pia kwa kuguswa na matatizo yetu na hatimae wameamua kuwekeza kwenye tasnia hii ya filamu, naomba management ya Proin Promotions isiangalie majina ya watu ndiyo wafanye nao kazi waangalie vipaji vya watu bila kujali madaraja kwamba huyu star au upcoming wawe tofauti na makampuni yaliyopo, wawe na tuzo kwa waliofanya vizuri kila mwisho wa mwaka na wasisikilize wasanii wanafiki watakaoenda kuwaponda wengine au kuwaharibia wenzao.

Rachel Haule:  Kiukweli mimi nimefurahi sana hasa kwa sisi ma-producer ni fursa nyingne na nzuri kwetu si unajua tena wasanii wote tunamtegemea muhindi tu! yaani binafsi namuomba mungu amsaidie huyu msambazaji ni imani akisimama atazidi kuleta mwanga kwa ma-producer.Na Treem Salim

IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA


TIMU ya soka ya mkoa wa Iringa imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0.
Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43.
Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59.
Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.

Shafii Dauda 'abaniwa' TFF, 40 wapitishwa kugombea


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBW3LXjv_QmCHQxtqq9JawR-pdTd0fZf6NVGgUx1dHgh4rbdA56YM212CcHPLdwQUZHpGuZyLuNsO3BG_1r66qliMu4RnMdv5iezj4RFhbpxc951ZB0YlOSIEgNa1CAX5aEydg50Yp5sk/s1600/shafi+dauda.JPG
Shafii Dauda aliyeenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF
 Na Boniface Wambura
Kamati ya Uchaguzi imepitisha majina ya waombaji 40 kati ya 58 kwa ajili ya uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utakaofanyika mwezi ujao.
Waliopitishwa katika orodha hiyo ya awali kwa upande wa Bodi ya Ligi ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).
Kwa upande wa Kamati ya Uendeshaji (Management Committee) ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi. Walioondolewa kwa vile si wenyeviti wa klabu za daraja la kwanza kama kanuni zinavyotaka ni Michael Njuweni Kaijage, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
Kanda namba moja (Kagera na Geita) aliyepitishwa kuwania nafasi ya ujumbe Kamati ya Utendaji ya TFF ni Kaliro Samson wakati Abdallah Hussein Musa ameondolewa kwa kutojaza fomu ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.
Jumbe Oddessa Magati, Mugisha Galibona na Vedastus Lufano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba mbili (Mara na Mwanza). Samwel Nyalla ameondolewa kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi wa TFF kwa kutoonesha malengo yake.
Waliopitishwa katika Kanda namba tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Swain a Mbasha Matutu wakati Stanslaus Nyongo ameondolewa kwa kukosa sifa ya uongozi wa angalau uzoefu wa miaka mitano kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.
Kanda namba nne (Arusha na Manyara) wamepitishwa wote watatu; ambao ni Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali. Kanda namba tano (Tabora na Kigoma) nao wamepitishwa wote; Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo.
Blassy Kiondo amepitishwa peke yake kuwania ujumbe Kanda namba sita (Katavi na Rukwa) huku Ayoub Nyaulingo aliondolewa kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
Naye Nazarius Kilungeja, Kamati ilikataa maombi yake ya kugombea ujumbe kutokana na vitendo vyake visivyo vya kimichezo ambavyo kwa kiasi kikubwa vilisababisha migogoro kwenye Mkoa wa Rukwa, hivyo suala lake litawasilishwa kwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.
Kanda namba saba (Iringa na Mbeya) waliopitishwa ni David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve na Lusekelo Elias Mwanjala. Cyprian Kuyava hakupitishwa kwa vile hana uzoefu wa uongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF huku Ayoub Shaib Nyenzi akiondolewa kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.
Elliud Peter Mvella ameondolewa kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa. Suala lake limewasilishwa katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.
Waliopitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge wakati Kamanga Tambwe ameondolewa kwa vile alipatikana na hatia ya kushiriki kwenye tuhumu za rushwa kwa waamuzi na kufungiwa na TFF.
Kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) waombaji wote watatu wameptishwa. Waombaji hao ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder. Pia waombaji wote wa Kanda namba kumi (Dodoma na Singida), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima na Charles Komba wamepitishwa.
Waombaji wanne kati ya watano wamepitishwa kwa Kanda namba 11 (Morogoro na Pwani). Waliopitishwa ni Farid Mbarak, Geofrey Nyange, Juma Abbas Pinto na Twahil Twaha Njoki.
Riziki Juma Majala ameondolewa kwa vile akiwa mtendaji mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) alishindwa kusimamia Kanuni za Ligi kwa kuruhusu timu ambayo si mwanachama wa wanachama wa COREFA kucheza ligi, hivyo kusababisha mgogoro mkubwa kiasi cha mwananchi mmoja kufungua kesi ya kusimamisha Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL). Suala lake litawasilishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.
Kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) wamepitishwa waombaji wote wawili. Waombaji hao ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.  Waombaji wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam).
Wagombea wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam).  Wagombea hao ni Alex Crispine Kamuzelya na Muhsin Said Balhabou.
Walioondolewa ni Omar Isaack Abdulkadir kutokana na vitendo vyake vya kutoheshimu na kutotekeleza maagizo ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. Atapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.
Shaffii Kajuna Dauda ameondolewa kwa kutumia nyaraka ya mawasiliano baina ya FIFA na Rais wa TFF bila idhini na kuiweka hadharani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, hivyo kukiuka maadili kwa kumiliki nyaraka ambazo hazikuwa kwenye mamlaka yake. Suala lake linapelekwa katika Kamati ya Maadili.
Naye Wilfred Kidao ameondolewa kwa kutumia nyaraka za Kamati ya Utendaji ya TFF bila ridhaa ya kamati, hivyo kukosa uadilifu. Suala lake linawasilishwa kwenye Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais, waombaji wote watatu wamepitishwa. Waombaji hao ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Wallace John Karia.
Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emil Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Rais. Omari Mussa Nkwaruro ameondolewa kwa kuwasilisha cheti chenye utata, hivyo kukiuka utashi wa Ibara ya 27(7) ya Katiba ya TFF. Pia aliwasilisha taarifa za uongo kuhusu uzoefu na kukiuka Kanuni za Maadili, hivyo suala lake linapelekwa Kamati ya Maadili.
Naye Richard Julius Rukambula ameondolewa kwa hakukidhi matakwa ya kugombea uongozi kwa mujibu wa Ibara ya 12(2)(e) ya Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kupelekwa katika mahakama za kawaida. Hivyo naye anapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua stahiki.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...