Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 1, 2014

HADIJA KOPA AWAPA BURUDANI YA NGUVU WAKAZI WA JIJI LA MBEYA


 Malkia wa Taarab nchini Bi. Hadija Kopa akiimba mbele ya umati wa watu kwenye ukumbi maarufu wa City Pub mjni Mbeya.
 Baadhi ya wanamuziki wa TOT Taarab wakiimba kwa hamasa wakati band hiyo ya muziki wa taarab ilipotumbuiza kwenye ukumbi wa City Pub mjini Mbeya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpongeza bi Hadija Kopa kwa umahiri wake wa kuimba taarab kwenye ukumbi wa City Pub Mbeya.
Umati wa watu ukiwa umefurika wakati Malkia wa Taaarab Hadija Kopa na Band ya Taarab ikitoa burudani kwa wakazi wa Mbeya mjini.

MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA,AACHIWA KWA KOSA LA KUZIDISHA MUDA KWENYE MKUTANO WAO WA HADHARA.


Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima  Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
 
MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA.

Na Denis Mlowe,Iringa

MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee walishikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa linalosemekana  kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

Kwa majibu wa Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helkopta na kuelekea mkoa wa Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Halima Mdee aliwataka wananchama wa Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
Alisema wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji hicho.
Mbowe alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo  wabunge na mwenyekiti wa chama katika mkutano  kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.



“Jeshi la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza walituachia huru na ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mbowe.

WAZIRI MKUCHIKA AGOMA KUMUONGELEA LOWASSA NA MBIO ZA URAIS 2015


Mwenyekiti  wa  CCM Taifa Rais Dr  Jakaya  Kikwete kushoto akimnadi Lowassa jimboni kwake katika uchaguzi mkuu wa mwaka  2010
 Waziri Mkuchika (kushoto) akihojiwa na mzee  wa matukiodaima leo mjini Iringa 
..................................................................................................................................................
HUKU  baadhi  ya  makundi  yakiendelea  kuibuka na kutoa kauli mbali mbali  dhidi ya waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kuwa ameanza kampeni za Urais mapema , waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) Ndugu George Mkuchika amesema  kuwa hajafanya  utafiti wowote juu ya Lowassa  hivyo hawezi  kuzungumzia chochote  kama ni rushwa ama lah.

Waziri mkuchika  alitoa kauli  hiyo mjini Iringa leo  wakati  akihojiwa wa wanahabari mara  baada ya  kumaliza kutoka hotuba yake ya maadili na Rushwa kwa watumishi  wa umma katika kikao cha kamati ya ushauri  (RCC) cha  mkoa wa Iringa  katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo .

Kwani  alisema Taasisi ya  kuzuiana na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini  imekuwa  ikiwakamata   watu na kuwafikisha mahakakani  bila  kuogopa kiongozi ama mtu wa chini na kuwa  utendaji wa taasisi hiyo  umekuwa ukiziongatia haki kwa kila mhusika.

Mkuchika  mbali ya  kugoma  kulizungumzia suala la Lowassa bado alisema  kuwa suala la Rushwa ni suala ambalo halikubaliki na kuziagiza Halmashauri  ya   wilaya  nchini  kuchunguza mienendo  ya  watumishi ambao waongoza  kwa kumiliki  mali mara  baada ya  kuingia serikalini  ili  kujua utajiri  huo wa haraka wanaotoa  wapi.

Hata  hivyo   akihojiwa  juu ya  sakata  ya aliyekuwa mshindi wa kura  za maoni ndani ya  CCM katika mchakato wa ndani ya chama hicho mwaka 2010 Frederick Mwakalebela suala lake kuchukua muda mwingi zaidi na kurudishwa mahakamani mara kwa mara  alisema ili kuwa si kwa lengo la kumuonea ila ilikuwa ni kutafuta sheria inasemaje katika  hilo na mahakani ndicho  chombo  pekee  cha kutafsiri sheria  hivyo maamuzi ya mahakamani siku  zote ni sahihi katika kutafuta  haki.


Awali Waziri Mkuchika  akihutubia katika ufunguzi wa kikao  hicho cha RCC alisema  kuwa  mikakati ya  ofisi yake  katika  kupambana na  watumishi  wasio na maadili ambao  wanashindwa  kufanya kazi  ya umma na  kutumia ofisi  za umma kujinufaisha  wenyewe.

Alisema kuwa  iwapo  watumkishi  wa umma hawatakuwa na maadili katika  uwajibikaji  wao  wa kila  siku ni  wazi suala la rushwa katika idara  wanazoongoza  zitaendelea   kuongezeka  hivyo  kuifanya  jamii  kuendelea  kuchukia serikali  yao.

Hata  hivyo  alisema ni  vema Halmashauri  kuhakikia  kamati za maadili ya  watumishi  zinafanya kazi vema  ili  kuwabaini  watumishi  wasio na maadili  katika Halmashauri  zao.

Pia  alisema serikali  kila mwaka  imekuwa ikipelekea fedha  zaidi ya asilimia 70 kwa Halmashauri kwa ajili ya manunuzi  ila matokeo  yake  badala ya  fedha  hizo  kutumika katika manunuzi wajanja  wamekuwa  wakizitumia kujinunulia mali  zao jambo ambalo alidai  halitavumilika katika wataki  huu.

" Haiingii akilini  kuna  mtumishi ameingia katika ajira  akiwa hana hata  gari  wala nyumba ila baada ya miezi  miwili ya  utumishi  wa umma unakuta  ana nyumba za kisasa, magari  na mali  nyingi ambazo mazingira ya upatikanaji  wake yanatia  shaka .....lazima  kuwa makini  sana na maofisa ardhi na  wakuu wengine  wa  idara "

Aidha  alisema katika  kukomesha  vitendo vya  rushwa katika Halmashauri ya idara  mbali  mbali za serikali  amewaagiza makamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU ) kuhakikisha  wanatoa  elimu kwa  mabaraza ya madiwani wa Halmashauri  zote nchini  ili  kuhakikisha vitendo vya rushwa  katika Halmashauri  vinakomeshwa.

Waziri Mkuchika  alisema  kuwa   hadi sasa kwa nchi zinazoongoza  kwa utawala bora katika  jumuiya ya  Afrika Mashariki   takwimu  zinaonyesha kuwa  kati ya nchi  tano  Tanzania ni nchi ya pili  kwa utawala  bora   .

Pia  alisema  chanzo  cha  mmomonyoko  wa maadili kwa mtumishi  wa umma  ni pamoja na tamaa ya mali  kwa  watumishi hao hali  inayosababishwa na kutoridhika na  kipato  halisi  wanachokipata pamoja na ubinafsi  wa kujitazama  wao badala ya  Taifa .

"Takwimu  kuhusiana na vita  dhidi ya  Rushwa  na  uwajibikaji kwa viongozi  unakabiliwa na changamoto  nyingi..... takwimu kuhusiana na vitendo  vya Rushwa  katika kipindi  cha kuanzia mwezi Julai 2012 hadi  Juni 2013 zinaonyesha  kuwa na jumla ya taarifa 81 zilipokelewa kati  ya hizo  65 zilifanyiwa kazi  uchunguzi  na kufunguliwa majalada .....aidha katika kipindi  hicho jumla ya kesi mpya 12 zilifunguliwa katika mahakama mbali mbali za mkoa wa Iringa na kesi 5 kati ya  hizo zilitolewa  hukumu na  wahusika kupewa adhabu mbali mbali" alisema waziri Mkuchika

Kuwa Halmashauri  ya  wilaya  pamoja na idara ya afya ndizo zinaongoza kwa kuwa na taarifa nyingi kwa upande wa idara za serikali  ambapo  kila moja ilipatikana na taarifa  16 huku idara ya mahakama  inafuatia kwa taarifa  6 wakati  polisi na idara ya  elimu zikiwa na taarifa 5 kila moja  idara ya maliasili taarifa  tatu  na idara ya mwisho kwa kuwa na taarifa  ndogo za rushwa ni idara ya ardhi  na  TANROADS ambayo ilikuwa na taarifa  moja ,Tanesco taarifa  moja,SIDO mbili,ofisi   ya mkuu wa wilaya  tatu ,na sekta  binafsi taarifa  tatu.

Mkuchika alisema kuanzia  sasa  maofisa wa Takukuru wilaya ya mkoa hakuna kushinda  ofisini na badala yake kwenda kwa  wananchi  kutoa elimu  ya Rushwa na  kuzitaka  taasisi mbali mbali zikiwemo za dini kutosita  kutoa taarifa kwa Takukuru  kuomba  maofisa  wake kufika na kutoa elimu katika mikusanyiko.

Mwenyekiti  wa Halmashauri ya  wilaya ya  Iringa Stephano Mhapa  mbali ya  kumpongeza  waziri Mkuchika kwa utaratibu  wake wa kuzunguka katika mikoa na kuzungumza katika vikao  vya RCC bado alimshauri  kufanya mikutano ya hadhara  kwa wananchi  zaidi ambao  ndio  wanaathiriwa  zaidi na rushwa ndogo  zinazoendelea  kutolewa na kuvuruga ubora wa  miradi.

Huku  mkuu  wa wilaya ya  Mufindi  Evarista  Kalalu  alisema  kuwa  mbali ya wilaya  yake ya Mufindi  kuongozana na maofisa wa TAKUKURU katika mikutano  yake wilayani ila bado  inapaswa TAKUKURU  kujipanga kwa  kutenga bajeti  ya  kufikisha  elimu zaidi kwa wananchi.

Kwani  alisema  iwapo  TAKUKURU haitakuwana nguvu zaidi  ya  kuwafikia  wananchi  wa pembezoni  zaidi  bado vita  dhidi ya  Rushwa  itaendelea  kuzungumzwa  pasipo  kueleweka  vema.

Mkuu  huyo wa wilaya  alisema Rushwa inayotesa wananchi ni ile inayotokana na uwajibikaji mbaya  wa  viongozi wa serikali  za vijiji na kata  ambao  ndio  wamekuwa  wakiongoza kwa  rushwa ndogo ndogo ambazo  zinaendelea  kutesa  wananchi .

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine  Ishengoma  aliwataka  watumishi  wote wa umma na  wananchi wa mkoa  wa Iringa  kushirikiana katika mapambano  dhidi ya  Rushwa kama  njia ya kuongeza kasi  ya maendeleo katika mkoa.

Dr Ishengoma alisema  kuwa iwapo  kila mmoja atajikita katika vita  dhidi ya  Rushwa mkoa  wa Iringa  unaweza kuwa mkoa wa mfano kwa maendeleo makubwa bila  Rushwa

Katika hatua  nyingine  mkuu  wa mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma  aliagiza Halmashauri zote za mkoa  wa Iringa ndani ya miezi mitatu  kuitisha  semina ya utawala  bora  katika  suala la Rushwa na maadili  kwa madiwani  wake.

"Mheshimiwa  waziri napenda kukuhakikishia  kuwa tunaye  kamanda wa TAKUKURU Mzuri  katika mkoa  wa Iringa japo kamanda nakuomba usije kutia  kiburi kwa waziri  wako  kutokana na sifa  hizi  ambazo  nimepata  kukupa hapa  leo"

Kamanda  wa Takukuru  mkoa  wa Iringa Bi Emma Kuhanga  alisema kuwa  mkoa  wa Iringa  umeendelea  kupambana na vitendo  vya  Rushwa na kuwa suala la  watumishi  wanaofika na kumiliki mali nyingi  habari zao wa kwanza  kuzibaini ni wakurugenzi na maofisa  utumishi ambao ndio  wamekuwa  wakijua mienendo  yao japo alisema bado  wataendelea  kufuatilia watumishi  wanaofanya vitendo  vya ufisadi kwa ajili ya kujilimbikizia mali katika mkoa

MKUTANO WA WADAU WA MASUMBWI LEO VIJANA KINONDONI


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masyumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akifatilia kwa makini mkutano wa Mabondia,mapromota na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi kulia ni bondia Sadiki Momba na Fabian Limo na mdau Maga kutoka Tegeta

Baadhi ya viongozi wakiwa meza kuu anae ongea ni Yasin Abdallah  kushoto ni Habibu Kinyogoli anaefati ni mwakilishi wa BMT Rais wa IBF Afrika Onesmo Ngoi na Lucas Retwainura

WADAU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA MASUMBWI



SKENDO ZA NGONO ZAWAZURIA JAMBO BONGO MOVIE KWA WAKATOLIK



hiyo ya Sister Marry.
KANISA la Romani Katoliki limeishukia tasnia ya filamu Bongo (Bongo Movies) kutokana na matendo maovu yanayofanywa na wasanii katika sinema zao hususan suala zima la kuheshimu imani za watu.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi amewaonya wasanii kuwa maigizo yao yasilenge kuchafua umma ama kikundi chochote kwani wanaweza kuleta mgawanyiko katika taifa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Cover la filamu h
Akifafanua zaidi kuhusiana na filamu hiyo, kiongozi huyo wa kiroho alisema alisononeshwa na kazi hiyo ambayo ilikuwa na dosari za kuingilia imani ya kikatoliki kwani mavazi ya kanisa yalitumika kuvaliwa bila staha.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.

Askofu huyo alisema taifa lina mambo mengi na linajivunia kwa amani ya muda mrefu, hivyo waigizaji hao wanapoigiza maigizo ambayo yanagusa imani au jamii ya watu wengine linaweza kuwa tatizo kubwa huko mbele.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.

MZEE GURUMO:MADEMU WANAJISOGEZA KWA DIAMOND




MSANII mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Muhidini Gurumo ambaye kwa sasa amestaafu, amefungukia skendo ya kuwa na mademu wengi inayomuandama Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni maeneo ya Ilala jijini Dar, Mzee Gurumo alisema: “Diamond ana nidhamu sana ila vile anavyotamba jukwaani na kudatisha mashabiki hapo ndipo balaa linapokuja, watoto wa kike wenyewe wanaanza kujisogeza kwake.
“Pamoja na skendo za mademu zinazomuandama, siwezi kumshusha thamani, ana haki ya kujiopolea mwanamke yeyote anayempenda, yeye kama mwanaume rijali wakati mwingine ni vigumu kujizuia na vishawishi hivyo.”

Promota jay msangi apigwa stop na serikali kuandaa mapambano ya ngumi



Shi....Shilole achia ngoma mpya iitwayo Chuna Buzi


Shilole
BAADA ya kutamba na kibao chake cha 'Nakomaa na Jiji', msanii Zuwena Mohammed 'Shilole' ameachia kazi mpya iitwayo 'Chuna Buzi' na kuwataka mashabiki wake kumuunga mkono kama walivyofanya katika kazi zake za nyuma kuanzia 'Lawama', 'Dume Dada' hadi 'Paka la Baa'.
Wimbo ni utunzi wa Barnaba Boy ambaye ameutendea haki kwa kum back-up mkali huyo anayekimbiza katika filamu pia.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AONDOKA KWENDA ZIARANI INDIA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake (katikati) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi  wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake,pichani akipeana mkono na Brigedia Jenerali Sheikh Sharif Othman .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

AZAM kukipiga na Ferreviario de Beira Chamazi



* CAF yaruhusu uwanja wake wa Chamazi

chamazi_2
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki  kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF kuchezewa mashindano ya kimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “kuchezewa mechi za CAF
Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripoti CAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechi zinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC umetoa shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazi na uweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC sasa imewatangazi
wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za  CAF zitachezwa Azam Complex Chamazi

BIBI KIZEE AKUTWA CHUMBANI KWA MTU NA KUHUSISHWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA LEO HUKO HAMUGEMBE MJINI BUKOBA


 Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi  amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu  akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya leo  Ijumaa Januari 31,2014 
 Bi. Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba. Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake  zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni  mchawi wakati wengine wakisema wasubili taarifa ya Polisi.
 
 Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na  Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
 Wakielekea kituo cha cha polisi cha Bukoba Mjini leo asubuhi.
 Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba
PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG

Yanga yakanusha Cannavaro, Niyonzima kuzichapa Mkwakwani


Niyonzima (kulia) na Cannavaro (kati) wakiwa na Chuji (24)

BENCHI la Ufundi la klabu ya Young Africans limekanusha taarifa kwamba nyota wawili wa timu yao, nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na Haruna Niyonzima 'Fabregas' walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa juzi jijini Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo wa www.youngafricans.co.tz , umemnukuu Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa 'Master' akisemataarifa hizo hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu twasira ya timu.
Mkwasa amesema benchi la ufundi wameshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na kuzisoma leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya maslahi yao tu.
Kila mtu alikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nashikwa wasi wasi na waandishi waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika kitu tofauti na walichokiona.
"Sheria za soka zipo wazi, mchezaji au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa kuwapa kadi nyekundu, sasa tumeshangazwa na taarifa hizo zilioripotiwa leo kuwa kuwa kuna wachezaji wetu walipigana ili wachezaji wote walicheza kwa dakika 90 "alisema Mkwasa.
Nadhani imefika wakati tuisaidie jamii kuelewa uhalisia wa jambo husika liliotokea, kwani kuandika tofauti na kilichotokea kunasababisha jamii kuamini/kuelewa jambo ambalo silo lililotokea.
Katika mchezo wowote wachezaji kuelekezana/kukumbushana majukumu ni jambo la kawaida na ndicho kilichotokea katika mchezo dhidi ya Coastal kati ya Cananavaro na Yondani na Niyonzima na Cannavaro na si kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hata mara baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa pamoja na kupeana pole kutokana na ugumu wa mechi, kisha wote kuondoka kuelekea hotelini kupumzika, na sisi kama viongozi hatujaona wachezaji kutofautiana kitu chochote hata kufikia hatua ya kusuruhishwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari " aliongeza Mkwasa .
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd "Chuji"  aliyekua amesimamishwa kurejeshwa kundini.

KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA


1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. 1AKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana Joseph Mwaisango.
3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
4Waendesha Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo. 5
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya kuwasili mkoani humo. 6Shangwe za waendesha bodaboda zikiendelea. 7
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 8
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi.

Bodi ya Ligi Kuu yazipiga jeki klabu za FDL


BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye akaunti za klabu husika. 

Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB zinatakiwa kuwasilisha haraka.
Klabu za FDL ni African Lyon, Burkina Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa JKT, Kimondo, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na Mwadui.
Nyingine ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro, Polisi Tabora, Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.

REX ENERGY YATAMBULISHA TEKNOLOJIA MPYA YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA UMEME


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia  mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard Rweikiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis Kibhisa wakiwaonesha na kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna moja ya kifaa cha kisasa kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Mwanga wa Jua (Solar).Kwa habari zaidi ingia www.rexsolarenergy.com
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi wa namna moja ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa katika suala zima la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power) mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis alibainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama vile taa,redio, friji, TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama nafuu.Pichani kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bwa.Medard Rweikiza akisikiliza
Baadhi ya  Wafanyakazi wa Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kumaliza mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi.

TFF mpya yatimiza siku 100 madarakani, Rais Malinzi kuteta Ijumaa


Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Na Boniface Wambura
KAMATI mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, Februari 4 mwaka huu inatimiza siku 100 tangu iingie madarakani katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28 mwaka jana.
Hivyo, Rais Malinzi atazungumza na waandishi wa habari Februari 7 mwaka huu kuelezea utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi. Muda na mahali utakapofanyika mkutano huo mtaarifiwa baadaye.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...