Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 29, 2014

KAMPUNI YA ISSERE SPORTS YATOA JEZI KWA SHULE YA SEKONDARI YA KEREZANGE


Mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo (Kushoto) akimkabidhi jezi namba 14 Mkuu wa Shule ya Sekondari Kerezange, Kivule Ilala Dar es Salaam, Bi. Kirundu Mgeni kwa niaba ya Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Isere kwa ajili ya timu ya soka shuleni hapo, Issere Sports ilitoa jezi mipira miwili na soksi (Picha na Mpigapicha Wetu) 

KAMPUNI ya kuuza vifaa vya michezo, Issere Sports imetoa jezi mipira na soksi kwa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Kerezange, iliyoko Kivule Ilala, Dar es Salaam.

Akikabidhi jezi hizo mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Issere, Abbas Ally alisema michezio inafanya wanafunzi kuondokana na maradhi.

Ufunguo aliyekubali kufundisha timu ya soka ya shule katika mashindano ya shule za Sekondari (UMISETA) alisema atatumia uwezo wake kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Mkuu wa Shule hiyo. Kirundu Mgeni alisema vifaa hivyo ni chachu ya wachezaji wa shule yake kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya wilaya yao ya Ilala.

Awali Mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Baraka Mololo alisema shule yake ina wachezaji wengi wenye vipaji ambao wakiendelezwa wanaweza kuchezea timu za Simba na Yanga na hata Taifa.

Alisema hivi karibuni shule hiyo ilifanya vizuri katika mashindano ya kirafiki na shule za jirani na kuibuka washindi hivyo ana matarajio makubwa ya kutwaa ubingwa wa UMISETA mwaka huu.

MKUTANO MKUU WA TASWA KUFANYIKA FEBRUARI 16


UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ulivyopangwa na Kamati ya Utendaji ya chama.
 
Hata hivyo sekretarieti ya TASWA imekubaliana kusogeza mbele muda wa kulipia ada kwa wanachama hadi Jumanne Februari 4 mwaka huu, badala ya Ijumaa Januari 31, 2014 iliyokuwa imepangwa awali, lengo likiwa ni kuwezesha wanachama wengi zaidi kulipia ada zao ili waweze kushiriki uchaguzi huo.
 
Wanachama wote walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ama 2010 au Mkutano Mkuu wa mwaka 2012 wana sifa ya kushiriki uchaguzi huo wanachotakiwa kufanya ni kulipia ada zao kuanzia mwaka 2011.
 
Malipo yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na hakuna mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama kwa sasa mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu.
 
Nawasisitiza wanachama kuhakikisha wanatumia vizuri muda uliobaki kwa kulipia ada zao ili waweze kushiriki mkutano huo. Kamati ya Uchaguzi ya TASWA inatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo kuzungumzia mambo mbalimbali yahusiyo uchaguzi huo.
 
 Nawasilisha.
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/01/2014.

YASSIN ABDALLAH ASHUKURU KAMATI YA UTENDAJI YA E&CAPBA


NDG ZANGU
    HIVI KARIBUNI VYOMBO VYENU KARIBU VYOTE VIMEWAFAHAMISHA WANANCHI WA TANZANIA JUU YA UTEUZI WANGU     WA  KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SHIRIKISHO KUBWA LA NGUMI ZA KULIPWA LA AFRIKA MASHARIKI .

NAPENDA KUTUMIA NAFASI HII KUISHUKURU KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO HILO ILIYOKUTANA JIJINI KIGALI-RWANDA KWA KUNIPATIA NAFASI YA KUWA MMOJA WA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU KATIKA SHIRIKISHO HILO,PIA NINAUPOKEA UTEUZI WANGU HUU KWA FURAHA KUBWA SANA.

NINA IMANI KUBWA SANA KUWA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO HILO IMETHAMINI MCHANGO WANGU AMBAO NIMEKUWA NIKIJITAHIDI SANA KUUTOWA KATIKA MCHEZO WA NGUMI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI,PIA MAHUSIANO MAZURI MIONGONI MWA VIONGOZI MBALIMBALI WA MASHIRIRIKA TOFAUTI YA NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI.

NIAAHIDI KWA UWEZO WA MWENYEZI MUNGU ATAKAONIJAALIA ,NITAJITAHIDI KUIMARISHA MAHUSIANO MEMA BAINA YA NCHI YANGU TANZANIA NA NCHI ZOTE ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KAMA AMBAVYO TAYARI VIONGOZI WETU WA JUU KITAIFA WAMESHAUANZISHA KWA KUUNDA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

WENZETU WA MPIRA WA MIGUU TAYARI WAMESHATUTANGULIA KWA KUUNDA CECAFA,NA TAYARI WANAFANYA MASHINDANO MAKUBWA YANAYOSIMIMIWA NA CECAFA ,NA YAMEONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA UHUSIANO BAINA YA NCHI NA NCHI.

NITAJITAHIDI KUSHAURIANA NA VIONGOZI WENZANGU WA SHIRIKISHO ILI KUANGALIA KWA UNDANI ZAIDI NI JINSI GANI TUNAWEZA KUUBORESHA ZAIDI MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ILI UWE NI AJIRA YA UHAKIKA KWA VIJANA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUPITIA MICHEZO.

                               MATATIZO YA VIJANA

TATHMINI INAONYESHA WAZI KWAMBA VIJANA NDIYO WAMEKUWA WAKITUMIWA KATIKA KUFANIKISHA MAMBO MENGI YA WATU,NA HATA KISIASA.KOTE DUNIANI

VIJANA WAMEKUWA WAKIHAMASISHWA KUSHIRIKI KATIKA MAANDAMANO YA KUZIPINGA SERIKALI ZILIZOKO MADARAKANI,NA WENGINE KUFIKIA KUPATA VILEMA VYA KUDUMU NA HATA KUPOTEZA MAISHA KWA FAIDA YA WANASIASA ,NA WAKISHAPATA MADHARA HAO WANAOWATUMIA HAWAWAPATII MISAADA YEYOTE NA HUISHIA MAGEREZANI,NA KUFANYISHWA KAZI AMBAZO URAIANI WANGEZIFANYA ,NA KUJIPATIA RIZIKI.KAMA WANGEWEZESHWA.

IKO HAJA KUBWA SASA KWA MAKAMPUNI MAKUBWA YA BIASHARA YA KUUTUMIA MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA AMBAZO ZIMEWATAJIRISHA SANA BAADHI YA MABONDIA DUNIANI NA KUWAPATIA UMAARUFU MKUBWA SANA KUTANGAZIA BIASHARA ZAO KWAKUUDHAMINI,MFANO; FLOYD MAYWEATHER NI MWANAMASUMBWI TAJIRI MIONGONI MWA WANAMICHEZO DUNIANI ,MANNY PAQUIAO YEYE NI MBUNGE WA PHILIPINES ,NA SASA VITALY KLYTCHKO HIVI SASA AMEINGIA KATIKA KINYANGANYILO CHA URAIS CHINI KWAKE UKREANE ,NA ANAITIKISA SERIKALI ILYOKO MADARAKANI .

NCHINI UGANDA BONDIA BINGWA WA ZAMANI WA WBF AMOT NYAKANA AMESHAWAHI KUSHIKA NYADHFA MBALIMBALI HATA YA UMEYA WA JIJI LA KAMPALA.

WOTE HAO NILIOWATAJA WAMEPATA UMAARUFU NA NAFASI WALIZONAZO  KUPITIA MCHEZO WA NGUMI.

PIA NAPENDA KUVISHUKURU VYOMBO VYENU VYA HABARI KWA USHIRIKIANO AMBAO MMEKUWA MKINIPATIA KATIKA UPASHANAJI HABARI ZA MCHEZO KWA MUDA WOTE NINAPOKUWA NA TAARIFA LAKINI PIA MNAPOTAKA TAARIFA KUTOKA KWANGU , MMENISAIDIA KUNIFANYA NIJULIKANE HATA NJE YA MIPAKA YA TANZANIA ,NA NINAKIRI KABISA YAWEZEKANA NYINYI NDIYO MMENITENGENEZEA NAFASI HII,MWENYEZIM MUNGU AWABARIKI WOTE.

KATIKA NAFASI HII MPYA NILIYONAYO HIVI SASA BADO NITAENDELEA KUVIHESHIMU VYOMBO VYOTE VILIVYOPEWA MAMLAKA YA KUSIMIMIA MICHEZO NCHINI TANZANIA ,IKIWEMO WIZARA YA HABARI UTAMADUNI ,VIJANA NA MICHEZO,KURUGENZI YA MICHEZO NCHINI ,NA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA[BMT] NA VIONGOZI WAKE WOTE, KAMWE SITOACHA KUOMBA USHAURI WAO KWA JAMBO LOLOTE LIHUSULO MICHEZO ,LIWE LA MAFANIKIO AU LA MATATIZO .


                                         imeletwa kwenu nami;
                                 yassin abdallah mwaipaya- ustaadh

LG yazindua aina ya OLED TV nchini Tanzania








Dar es Salaam, tarehe 29 January 2014 – LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.
TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.  
 TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”
TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.
Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.
Hii itampa mteja  uonaji mzuri isiyokuwa na mwisho. Burudani ya nyumbani imejazwa na mabadiliko yanayo endelea kila siku na sisi kama kampuni ya LG ni kazi yetu kuwa letea bidhaa inayoendana na wakati huu”
Mtengenezaji kutoka Korea ya Kusini amekaririwa akisema kuwa utendaji waLG 55EA9800 una kasi mara mia zaidi ya TV zingine aina ya LED/LCD, ambayo inaweza kupunguza mwanga wa picha zinazo jionesha kwa kasi katika kioo cha TV
Kampuni ya LG imeongeza‘rimoti ya ajabu’yenye uwezo wa kupokea sauti na ishara na mchanganyiko wa mambo mbali mbali.

CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO WALIYOPATA


Nape akizungumza na  wanahabari  mkoani Mbeya leo 
..............................................
Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”

Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.

Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.

Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.( Stori na Picha Adam H. Mzee)

MTEMVU AZINDUA BONANZA LA MAVETERANI YOMBO MAKANGARAWE, TEMEKE


 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Matemvu akikagua timu ya Veterani ya Yombo Kilakala wakati wa uzinduzi wa michuano ya maveterani ya Ujirani Mwema, katika Kata ya Yombo Kilakala, Temeke, Dar es Salaam juzi. Timu 12 kutoka sehemu mbalimbali za jiji zilishiriki kwenye michuano hiyo. Timu hiyo ilicheza na Kigamboni Veterani.
 Mtemvu akikagua timu ya Kigamboni Veterani. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makangarawe, Victor Mwakasendile.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtemvu akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo aliahidi kuyadhamini kwa timu zote kuzinunulia jezi za TMK. Kushoto ni Mwakasendile na Mungia Mbwana mratibu wa michuano hiyo.
 Timu za New Kivule Veterani (waliovaa Bluu) na Kitunda (waliovaa bluu nyeusi) wakipepetana
 Ni mtanange kwa kwenda mbele
 Hapiti mtu hapa
 Sasa nawatoka
 Wanachi wakishuhudia mpambano huo
 Timu za Yombo Makangarawe Veterani (BLUU)  wakicheza na Kigamboni Veterani huku wananchi wakishuhudia
 Mlinda mlango wa Kigamboni akiwania mpira na mchezaji wa Yombo Makangarawe

Rais aagiza Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. 
Picha na Freddy Maro wa Ikulu. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.

Rais pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.

Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza kujitegemea tena.

Rais Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.

Katika hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao wanalala, Rais Kikwete amesema   ameagiza
Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.

“Kazi yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo
maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: 
“Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.” Kuhusu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa
Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutoshana hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. 

Tutahakikisha kuwa yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini na waje kupata vichomi.”                        Kuhusu maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye makambi.

Rais ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.

                        “Hili ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.” 

Soma Taarifa Kwa Umma Kutoka Kwa Mwenyekiti, Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Juu ya Deni la Taifa na Uteuzi wa Waziri Mpya wa Fedha

 

 Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Mwenyekiti, Chama Cha Wananchi CUF.
---
CHAMA CHA WANANCHI(CUF)

Rais Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri baada ya Mawaziri wanne kuachishwa kazi kutokana na kashfa ya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu uliotokea katika Operesheni Tokomeza na kifo cha Waziri wa Fedha. Katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Kikwete hakuzingatia malalamiko ya Sekretariati ya CCM kuwa Mawaziri Mizigo wanakiathiri chama CCM hususani wakati huu tukielekea katika uchaguzi mkuu 2015.

Mawaziri walioanishwa na Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi wa CCM kuwa ni mizigo na kuhojiwa na Kamati Kuu ya CCM na ambao wamebaki katika Baraza la Mawaziri ni pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Elimu), Christopher Chiza (Kilimo), Dk Abdallah Kigoda (Viwanda), Celina Kombani (Utumishi wa Umma) na Hawa Ghasia (Tamisemi). Mhe. Saada Mkuya Salum akiwa Naibu Waziri alihojiwa kwa niaba ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa ambaye kwa sasa ni marehemu. Rais Kikwete amemteua Mhe. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi.

Waziri wa Fedha na Uchumi ndiyo msimamizi mkuu wa sera za uchumi za nchi. Ana majukumu ya kusimamia uandaaji wa bajeti ya serikali ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada ya sera za kodi na kuzitekeleza, kuandaa makadirio ya matumizi ya serikali na kusimamia utekelezaji wake baada ya kupitishwa na Bunge. Sera za serikali kupitia wizara ya fedha ni nyezo muhimu ya kukuza uchumi kwa kuhakikisha kuwa matumizi ya serikali yana tija ya juu, kuongeza ajira, kuhakikisha sekta za jamii hususan afya na elimu zinatengewa fedha za kutosha, kudhibiti mfumko wa bei kuhakikisha nchi ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, kudhibiti ongezeko la deni la taifa, kuhakikisha idara na mashirika ya serikali yanawajibika katika matumizi yao ya fedha za umma.

Waziri wa Fedha ndiye anayeongoza majadiliano na mashirika ya kimataifa yanayohusu sera za uchumi, fedha, misaada na mikopo kama vile Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Misaada ya Nchi zilizoendelea kama vile DFID (Uingereza), SIDA (Sweden), DANIDA (Denmark), USAID na MCC (Marekani) na kadhalika.

Tanzania imeanza kukopa katika masoko ya biashara kwa kasi na ari mpya. Waziri wa Fedha ana wajibika kuweka break nchi isije ikajikuta ina madeni isiyoweza kuyalipa.

Ndani ya serikali kuna mivutano mikubwa kati ya wizara ya fedha na wizara, idara na mashirika mengine. Kila wizara inataka itengewe fedha zaidi. Wizara ya fedha lazima isimamie matumizi yasizidi mapato. Waziri awe na uwezo wa kupambana na Mawaziri wenzake ambao wanakiuka bajeti zao. Awe na ujasiri wa kumueleza Rais kwa heshima na taadhima ofisi yake izingatie bajeti iliyopitishwa. Kuna taarifa kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, Ofisi ya Rais ilitumia zaidi ya bajeti ya mwaka mzima ya safari za Rais. Waziri wa Fedha anapaswa kumueleza Bosi wake kwamba sote tunawajibika kuheshimu bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Waziri wa Fedha ndiye kiranja wa asasi nzito kama vile Benki Kuu BOT, Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Amana (Capital Markets and Securities Authority), Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (Public Procurement Regulatory Authority), Idara ya Usimamizi wa Bima (Insurance Supervisory Department), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (National Board of Accountants and Auditors) na kadhalika.

Wizara ya Fedha ndiyo inayosimamia hisa za serikali katika kampuni kama vile National Microfinance Bank (NMB), Tanzania Investment Bank (TIB), National Bank of Commerce (NBC), Tanzania Postal Bank (TPB), National Insurance Corporation (NIC) na mashirika mengine ya Umma. Wizara ya Fedha inasimamia mifuko ya Pensheni ikiwemo Public Service Pension Fund, Parastatal Pension Fund na Government Employees' Provident Fund.
Waziri wa Fedha anastahiki kuwa na uelewa na uwezo mkubwa wa kuchambua sera za uchumi, kujenga hoja wakati wa majadiliano na mashirika ya kimataifa, kuweza kuonyesha uongozi katika mijadala na mawaziri wenzake na asasi nyeti kama vile Benki Kuu.

Rais Kikwete amemteua Mhe. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Fedha baada ya kifo cha Dr William Mgimwa. Uteuzi wa mwanamke kuwa Waziri muhimu ni jambo jema katika kupambana na mfumo dume. Mhe. Saada ni Mzanzibari. Moja ya kero za Muungano ni kuwa Wazanzibari hawapewi fursa kuongoza wizara muhimu kama vile Wizara ya Fedha. Mhe. Zakhia Meghji ambaye aliteuliwa na Rais Kikwete baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Fedha. Haidhuru yeye pia ana asili ya Zanzibar lakini alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. Kashfa ya uchotaji wa fedha za EPA Benki Kuu ilimlazimisha ajiuzulu. Kumteua Saada Mkuya Salum kuwa waziri kunaua ndege wawili kwa jiwe moja. Ni mwanamke na Mzanzibari wa Zanzibar.

Wasifu wa Mhe. Saada Mkuya Salum uliowekwa katika tovuti ya Bunge unaonesha kwa Mhe.Saada alijiunga na CCM mwaka 2000 na yeye ni mwanachaama wa kawaida. Bi Saada alimaliza kidato cha 6 mwaka 1995 Sekondari ya Lumumba Zanzibar. Shule ya Msingi alisomea Kisiwandui na sekondari ya kawaida (O level) alisomea Hamamni. Mwaka 1997 – 99 alifanya masomo ya biashara na akatunukiwa sitashahada ya juu. Kati ya 2000 – 2002 alifanya masomo ya shahada ya pili ya biashara (Courses for the Second Degree in Business) na akapata cheti (certificate). CV imetaja shule ya msingi alizosomea lakini vyuo alivyosomea havikutajwa.

Alianza kufanya kazi Hazina Zanzibar mwaka 2003 kama afisa. Mwaka 2006 alikuwa Afisa Tawala (Administrative Officer). Kati ya mwaka 2008 na 2010 alisomea shahada ya Master of Finance. Chuo alichosomea hakikuelezwa. Kutotaja Chuo kunaweka wasiwasi wa ubora wa shahada aliyoipata. Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Kamishna wa Fedha (Commissioner of Finance) na Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha. Baadhi ya Wabunge niliyozumgumza nao wamenieleza kuwa Mhe. Saada amefanya kazi nzuri Bungeni hasa katika kipindi ambacho Marehemu Dr Mgimwa alikuwa mgonjwa.

Ikiwa wasifu uliobandikwa katika tovuti ya Bunge ni sahihi ni wazi Mhe. Mkuya hana uzoefu wa kisiasa, kitaaluma na kiutawala wa kuongoza Wizara nzito na nyeti. Sina uhakika ana uelewa wakutosha kuhusu menejimenti ya fedha za umma (Public Financial Management), upembuzi yakinifu wa miradi ya umma, athari za nakisi ya bajeti katika mfumko wa bei, deni la taifa na upatikanaji wa mikopo kwenye sekta binafsi. Sera muhimu ya kukuza na kubadilisha mfumo wa uchumi, hususani kuendeleza viwanda vya ndani, kuongeza uuzaji wa bidhaa nchi za nje na hivyo kuongeza ajira ni kuwa na thamani halisi ya sarafu (real exchange rate) yenye kuongeza ushindani katika soko la dunia. Kuongezeka kwa tija na ufanisi katika uzalishaji bila kubadili thamani ya shilingi kunaongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la dunia. Mfumko wa bei unapunguza ushindani wa bidhaa za Tanzania ndani ya nchi na kwenye soko la dunia na hivyo kuathiri ongezeka la ajira. Sera za riba na upatikanaji wa mikopo ni suala muhimu katika kuendeleza uwekezaji ambao utakuza uchumi na kuongeza ajira.

Serikali inakabiliwa na matatizo makubwa ya fedha. Matumizi yanaongezeka kwa kasi kubwa kuliko mapato. Bajeti inayowasilishwa na serikali Bungeni imekuwa na makadirio makubwa ya mapato kuliko ukusanyaji halisi. Matumizi ya kawaida yanaongezeka kwa kasi kubwa na kupunguza uwezo wa serikali kuchangia katika Bajeti ya Maendeleo.
Nakisi ya bajeti imeongezeka toka shilingi bilioni 389 mwaka wa 2007/08 sawa na asilimia 1.7 ya pato la taifa na kufikia shilingi bilioni 2992 mwaka 2012/13 sawa na asilimia 6.2 ya pato la taifa. Mwaka huu wa fedha 2013/14, bajeti imeishafumka. Mapato ni madogo kuliko makadirio. Matumizi ni makubwa. Serikali inalimbikiza madeni kwa makampuni yanayoiuzia bidhaa na huduma.

Serikali imekuwa inakopa katika masoko ya kibiashara kwa gharama kubwa na deni la taifa linaongezeka kwa kasi. Deni la taifa limeongezeka toka shilingi trilioni 5.9 mwaka 2007 sawa na asilimia 28.4 ya pato la taifa na kufikia shilingi trilioni 22 mwaka 2013 sawa na asilimia 42.5 ya pato la taifa. Tukiendelea na kasi hii ya kukopa Rais Kikwete ataiachia nchi tatizo kubwa la deni la taifa na hasa deni la nje.

Katika sekta ya ujenzi wa barabara kuna tatizo kubwa la makandarasi wengi kutolipwa kwa wakati na hivyo kucheleweshwa kukamilishwa kwa miradi. Wakati mwingine Wizara ya Ujenzi inatia sahihi miradi mipya hata kama hakuna fedha zilizotengwa ndani ya bajeti. Waziri wa Fedha ana wajibu wakuweka nidhamu katika matumizi ya serikali. Awe na uwezo wa kumueleza Waziri Magufuli asiweke sahihi miradi mipya ya barabara ambayo haijatengewa fedha.

Uendeshaji wa TANESCO una gharama kubwa katika bajeti ya serikali. Tanesco ilipata hasara ya dola milioni 240 na ina limbikizo ya madeni ya dola milioni 276

Katika kipindi hiki tuna mchakato wa katiba mpya ambao una gharama zake. Bunge la Katiba litaanza kukutana mwezi Februari. Bunge litafuatiwa na Bunge la Bajeti. Tume ya Uchaguzi inawajibika kuboresha Daftari la Wapiga kura kabla ya kura ya maoni. Tume haijaboresha daftari kwa sababu ya kukosa fedha. Uandikishaji wa vitambulisho vya taifa unasuasua kwa kutokuwa na fedha za kutosha.

Katika kipindi cha kueleka uchaguzi mkuu nidhamu ya matumizi ya serikali inatoweka. Rais na wapambe wake wanafikiria taratibu za maisha baada ya kuondoka Ikulu. Kuna kuwa na shinikizo kubwa za misamaha ya kodi na mikataba inayoweza kuwanufaisha katika kipindi cha kustaafu. Kuna shinikizo ya kupata fedha za kusaidia Chama Tawala wakati wa uchaguzi. Katika kipindi cha pili cha Rais Mkapa akielekea kun’gatuka aliuza nyumba za serikali kwa bei poa kwa mawaziri, viongozi wa CCM na watumishi wa serikali. Kashfa ya kuchota fedha za EPA ilitokea wakati tukielekea uchaguzi wa 2005. Waziri wa Fedha anawajibika kupambana na shinikizo hizo.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mwaka 2005, Mhe. Kikwete alieleza kuwa hakuna Chuo kinachofundisha Uwaziri kwa hiyo yeyote anaweza kuwa Waziri. Bila shaka mtazamo huu unachangia kuteua Mawaziri Mizigo wasiyokuwa na sifa au uwezo wa kutekeleza majukumu yao. Chanzo cha tatizo siyo Mawaziri Mizigo bali ni Rais Mzigo anayetokana na Chama mzigo.

Watanzania tunakabiliwa na matatizo ya gharama kubwa za maisha, ukosefu wa ajira, elimu duni, huduma mbovu za afya, kukithiri kwa rushwa na utawala mbovu. Tunapaswa kujipanga kukiondo Chama Mzigo madarakani.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti, Chama Cha Wananchi CUF.

UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM UDIWANI KATA YA NDULI IRINGA


 Mgombea udiwani  kata  ya  Nduli   jimbo la Iringa mjini  kupitia  chama cha mapinduzi (CCM) Benitho Mtove akiwatambulisha  katika uzinduzi wa kampeni juzi  waliokuwa washindani  wenzake  katika  kinyang'anyiro  cha kura  za maoni  ndani ya  CCM kabla ya  kuwashinda (picha na Francis Godwin Blog)
  Katibu  wa CCM wilaya ya  Iringa mjini na kaimu katibu wa mkoa  wa Iringa Hassan Mtenga akimwagiza mstahiki  meya  kufuatilia fedha za mfuko wa  jimbo la fedha zinazotolewa na  wafadhili kwa mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji peter Msigwa kwa ajili ya  wananchi wa  jimbo  hilo juzi (picha na Francis Godwin Blog)
 Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu  akimwombea kura  mgombea  udiwani wa CCM kata ya  Nduli Bw Benitho Mtove (hayupo pichani) juzi wakati  wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kata ya Nduli (picha na Francis Godwin Blog)
 
Aliyekuwa  mshindi wa kura  za maoni ndani ya  CCM mwaka 2010 Frederick Mwakalebela akimwombea  kura  mgombea  udiwani wa CCM kata ya Nduli Bw Benitho Mtove  wakati wa mkutano wa  uzinduzi wa kampeni  za CCM juzi (picha na Francis Godwin
  Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) akimnadi mgombea wa udiwani wa Chadema kata ya Nduli Ayub Mwenda (kulia) siku ya  uzinduzi wa kampeni za Chadema kata  hiyo ya nduli katika viwanja hivyo hivyo ambavyo CCM imezindua kampeni  zake (picha na Francis Godwin Blog)


 Sehemu ya  wananchi  wa  Nduli  wakimsikiliza mbunge Mchungaji Peter Msigwa wakati wa uzinduzi huo wa kampeni za udiwani  Chadema kata ya Nduli (picha na Francis GodwinBlog)

M4C OPERESHENI PAMOJA DAIMA NDANI YA IRINGA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa jana.
Maelefu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesheni ya M4C Pamoja Daima wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana. (PICHA NA CHADEMA)

Rais aagiza Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. 
Picha na Freddy Maro wa Ikulu. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.

Rais pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.

Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza kujitegemea tena.

Rais Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.

Katika hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao wanalala, Rais Kikwete amesema   ameagiza
Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.

“Kazi yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo
maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: 
“Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.” Kuhusu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa
Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutoshana hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. 

Tutahakikisha kuwa yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini na waje kupata vichomi.”                        Kuhusu maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye makambi.

Rais ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.

                        “Hili ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.” 

Monday, January 27, 2014

MASHINDANO YA MKOA DAR ES SALAAM YAANZA ILALA



Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindan ya  wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es salaam DABA akimkabidhi risara Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu wakati wa mashindano ya wazi yaliyoanza jumatatu

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kulia  akimtupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akifatilia mchezo wa ngumi
Na Mwandishi Wetu

SHILIKISHO la ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tangia waingie Madarakani mashindano hayo yalifunguliwa jana na mgeni rasmi


Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ambayo imekutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huu akisoma risala kwa mgeni rasmi 


Mwenyekidi wa ngumi mkoa wa Dar Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changanmoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye karenda yao ata hivyo akuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la ilala tunaomba utupatie angarau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo avikizi kimchezo


akijibu lisara hiyo mbunge huyo ame haidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele 


katika ufunguzi huo mabondia Anton Idoa alimtwanga kwa K,O ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said, na shabani Alimasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya shanti ya Ilala,Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi na Ayubu Ibrahimu  
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...