Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dk. Dr.Israel Mwakyolile akipokea hundi za fedha zenye thamani ya shillingi millioni 60 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juuu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. Kushoto ni Askofu Isaya Mengele wa Jimbo la Njombe . Jumla ya Shillingi Millioni 120 zilipatikana katika harambee
hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei akikabidhi picha yake kwa Ndugu Boimanda aliyenunua kwa Shillingi Millioni mbili katika harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juuu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. Jumla ya sh. milioni 120 zilipatikana amabapo benki ya CRDB ilichangia shillingi millioni 65. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dr. Dr.Israel Mwakyolile na kulia ni Askofu Isaya Mengele wa Jimbo la Njombe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei akivishwa heshima ya uchifu wa mikoa ya nyanda za juu kusini na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri jimbo la Njombe Askofu Isaya Mengele baaada ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juuu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. Jumla ya sh milioni 120 zilipatikana amabapo benki ya CRDB ilichangia shillingi millioni 65.
MBEYA, Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei juzi aliongoza harambee ya uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Mbeya ambapo jumla ya sh.120 millioni zilipatikana.Benki ya CRDB ilichangia jumla ya shillingi millioni 65 katika harambee hiyo.
Kwa kuonyesha shukrani zao kwa msaada huo, wazee wa mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri dayosisi ya Konde Askofu Dk.Israel Mwakyolile walimvika Dk.Kimei hadhi ya uchifu wa makabila ya mikoa ya Kusini na Nyanda za juu.
TUNAMSHUKURU SANA DR CHARLES KIMEI KWA KUTUTIA MOYO KATIKA HARAMBEE YA UANZISHWAJI WA CHUO KIKUU CHA NYANDA ZA KUU KUSINI.
ReplyDelete