Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 19, 2012

KUTOKA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA:Kufuatia Ajali ya Meli Zanzibar, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Yasitisha Mikutano ya Kukusanya Maoni Kusini Pemba


 Bi. Aziza Mcha, mkazi wa Kijiji cha Mtende, Wilaya ya Kusini Unguja akikabidhi karatasi yenye maoni yake kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Yussuf Mshamba hivi karibuni katika mkutano uliofanyika katika shule ya Mtende.Picha na Othman Maulid

Alhamisi, Julai 19, 2012
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa ya ajali ya Meli ya MV SKAGIT iliyotokea jana, Jumatano, tarehe 18,  Julai  2012 katika eneo la Chumbe, Zanzibar.
Kutokana na msiba huu mkubwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatoa Taarifa kwa Wananchi kuwa imesitisha Mikutano ya kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya iliyokuwa inaendelea katika Mkoa wa Kusini Pemba. Mikutano iliyositishwa ni ile iliyopangwa kufanyika kuanzia leo, Alhamisi, Julai 19, 2012 hadi Jumamosi, Julai 21, 2012 katika maeneo ya Wawi, Vitongoji, Chanjamjawiri, Pujini, Gombani na Wara.
Zoezi la kukusanya Maoni litaendelea kuanzia  Jumapili tarehe 22, Julai, 2012.  Ratiba ya Mikutano katika maeneo yaliyositishwa itatolewa baadaye.
Tume ya Mabadilikio ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa mabadiliko haya hayahusu mikutano ya kukusanya maoni inayoendelea kufanyika katika mikoa sita (6) ya Tanzania Bara ambayo ni Pwani, Tanga, Dodoma, Shinyanga, Kagera na Manyara.  Tume inawaomba wananchi wa Mikoa hii kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao.
Mwisho, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatoa pole kwa wafiwa, majeruhi na wote walioguswa na ajali hii na tunamuomba Mwenye Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na majeruhi wote wapone kwa haraka.
Imetolewa na:
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
S.L.P. 1681,
DAR ES SALAAM,
Simu: 2137833,
Simu ya Mkononi: 0757 500800

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...