Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 9, 2012

LULU AZIDI KUSOTEA KESI YA KUDAIWA KUMUUA KANUMBA





Lulu akiwa kortini
Lulu kabla ya kukumbwa na mkasa unaomuandama kortini.
Msanii Eizabeth Michael maarufu kwa jina la ‘Lulu’ anaendelea kusota mahabusu baada ya Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuahirisha tena kesi inayomkabili ya mauaji dhidi ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

Leo, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilisogeza mbele tarehe ya kusikiliza maombi ya kufanya uchunguzi wa umri halisi wa Lulu hadi Julai 23 mwaka huu.

Jaji Dk. Fauz Twaib alisema mahakama yake imepokea waraka kutoka Mahakama ya Rufani Tanzania wa kuitisha jalada la kesi hiyo kwa ajili kuipitia, hatua iliyotokana na maombi ya upande wa Jamhuri.

Jaji Dk. Twaib alisema kuwa kutokana na kuitishwa kwa jalada hilo na Mahakama ya Rufani, mahakama yake haitasikiliza kesi hiyo hadi jalada litakaporejea.

Kabla ya hapo, upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani ukitaka ifanye mapitio ya kesi hiyo kuhusu uamuzi uliotolewa na Jaji Dk. Twaib kukubali kusikiliza maombi ya Lulu na pande zote mbili ziliamriwa kuwasilisha vielelezo dhidi ya maombi hayo ya kutaka kuchunguzwa kwa umri halisi wa Lulu. Upande wa Jamhuri ulipeleka maombi Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Jaji Dk.Twaib kusikiliza maombi hayo.

Katika maombi ya upande wa utetezi, mshtakiwa anadai kuwa umri wake ni miaka 17 na sio miaka 18 kama ilivyoandikwa kwenye hati ya mashtaka na hivyo ameomba Mahakama Kuu kuchunguza utata huo na kutoa uamuzi.

Katika kesi hiyo, Jamhuri inawakilishwa na mawakili wa serikali, Shadrack Kimaro na Elizabeth Kaganda, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na mawakili Florence Massawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama.

Kwenye kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa alimuua Kanumba Aprili 7 mwaka huu, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Nafikiri kwa swala la lulu, umri sio idadi ya miaka aliyoishi bali ni mambo anayo yaweza. Picha hapo juu inaonyesha ni katoto kamekaa juu ya bar counter ambapo kanaonekana kanaweza offer any service hata kumshinda mtu mzima

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...