Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 4, 2012

NHC YASAINI MIKATABA YA BILIONI 165/- NA MABENKI KWA AJILI YA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limesaini mikataba ya mkopo wa Sh bilioni 165 kutoka kwa taasisi tisa za fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba pamoja na ununuzi wa ardhi ya akiba.

Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika leo Dar es Salaam baina ya shirika hilo  na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambapo hali hiyo ilielezwa kuwa moja ya hatua zinazofanywa na NHC katika kutafuta mitaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi.

Taasisi za fedha zilizotoa  mkopo huo pamoja na kiwango walichotoa kwenye mabano ni pamoja na CRDB (Sh bilioni 35), ECO Bank (Sh bilioni 2), TIB (Sh bilioni 22), BancABC  (Sh bilioni 4.2), NMB (Sh bilioni 26), CBA (Sh bilioni 24), LAPF (Sh bilioni  15), Azania (Sh bilioni saba) na Shelter Afrique (Sh bilioni 23).

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa  NHC, Nehemia Mchechu alisema shirika hilo limekopa kiwango hicho cha fedha bila udhamini wowote wa serikali ambapo hali hiyo inatokanana utendaji wa kuridhisha wa shirika.

Alisema kutokana na mkopo walioupata wataanza kutekeleza mradi wa kujenga nyumba 15,000 ambazo ni kwa ajili ya watanzania wa kipato cha kati na juu lakini pia wakijikita zaidi kujenga nyumba za bei nafuu.

“Kutokana na mkopo huu shirika litajenga nyumba za bei nafuu zinazoanzia sh milioni 25 na zaidi hadi kufikia sh milioni 200,” alisema Mchechu na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha na imani na watanzania.

Alisema mkopo walioupata mrejesho wake ni wa aina tofautitofauti kwani upo ambao ni wa miaka minne na hadi miaka 10 nakwamba utekelezaji wa ujenzi umeanza kutekelezwa katika maeneo  mbalimbali nchini kama mikoa ya Dar es Salaam,Kigoma,Arusha na Dodoma.

Kuhusu ujenzi wa nyumba nafuu alisema upembuzi yakinifu unaendelea nchi nzima kuzitambua wilaya ambako miradi hiyo ya nyumba za bei nafuu itaanzia.

Hata hivyo alisema NHC inahitaji fedha zaidi kwa ajili ya kujenga miji mipya katika maeneo yaliyokwishatambuliwa ambayo ni Mateves-Burka (Arusha), Kawe(Dar es salaam), Usa River (Arusha) na Temeke
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema maendeleo ya miji huhitaji fedha nyingi ndio maana NHC imeona ianze na kujenga nyumba ili watanzania wasihangaike.

Alisema mikopo hiyo inalipika na lengo kubwa ni kuhakikisha nyumba zitakazojengwa zitakuwa za bei nafuu ambapo itasaidia shirika hilo kutekeleza miradi yake ya ujenzi ukiwemo ule wa kujenga nyumba 15,000 ifikapo mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...