Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 2, 2012



 
TIMU ya mchezo wa pool ya Spaider, juzi ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012' baada ya kuibamiza Tanga Beathing magoli 13-7 katika mchezo wa fainali za mashindano hayo ngazi ya mkoa wa Tanga.
Mashindano hayo ambayo yalichezwa kwa siku nne mfululizo yalikuwa yakifanyikia kwenye ukumbi wa baa ya Mangroove iliyopo Sahare mkoani hapa.
Spaider kwa kutwaa ubingwa huo mbali ya kujinyakulia fedha taslim Sh.700,000 pia ilikata tiketi ya kuwa mwakilishi wa mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika Septemba mkoani Mwanza kwa kushirikisha timu 16 ambazo zitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao
Tanga Beathing kwa kushika nafasi ya pili ilizawadiwa Sh.350,000 wakati ambapo Michael Pub yenyewe ilipewa Sh.200,000 baada ya kushika nafasi ya pili kufuatia kuibuka na ushindi wa magoli 13-12 dhidi ya Member Of Family katika mchezo wa kutafuta nafasi ya tatu. Member iliondoka na Sh.100,000 kwa kushika nafasi ya nne
Timu za Ngamiani, Kange Brothers, Highway na Kijiti zenyewe kila moja ilipewa kifuta jasho cha Sh.50,000 kila moja kufuatia kuingia robo fainali ya mashindano.
kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Sango Jerry wa timu ya Member Of Family alitwaa ubingwa huo kupata nafasi ya kuwaukilisha mkoa huo katika fainali za taifa kwa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) na pia alizawadiwa Sh.350,000 baada ya kumchapa mpinzani wake, Mohamed Simtoe wa timu ya Spaider magoli 2-0 katika mchezo wa fainali.
Simtoe aliyeshika nafasi ya pili alipewa Sh.200,000, wakati ambapo Ibrahima Abeid wa timu ya Spaider alishika nafasi ya tatu na kuondoka na Sh.150,000 na Abeid Juma wa timu ya Ngamiani yeye alishika nafasi ya nne na kupewa Sh.100,000.
Halima Hamisi kwa upande wa (wanawake) wa timu ya Spaider yeye naye alipata nafasi ya kuuwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa baada ya kutwaa ubingwa huo na pia kuondoka na Sh.250,000, Tima Abbas wa Spaider pia alishika nafasi ya pili na kupewa Sh.150,000, zainabu Omary wa timu ya Highway aliibukia katika nafasi ya tatu na kupewa Sh.100,000 na Fatma Ballo alishika nafasi ya nne na kuzawadiwa Sh.50,000.
Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo mkoani hapa, Zahoro Ligalu ambaye ni mweka hazina wa chama cha mchezo huo nchini (TAPA).
Mwekahazina wa chama cha mchezo wa pool Taifa Zaholo Ligalu (kulia) akimkabizi kitita cha pesa taslimu laki saba Nahoza wa timu ya Spaida, Ibrahimu Abedi baada ya timu yake kuchukua ubingwa wa mashindano ya Pool Safari Lager Mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki.Katikati ni katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Mashaka Muhando.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...