Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 16, 2012

TIMU YA SIMBA YABAMIZWA GOLI 2.0


 Mshambuliaji wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Dany Mrwanda (kulia) akichuana kuwania mpira na Nahodha wa URA ya Uganda, wakati wa mchezo wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo timu ya Simba imefungwa mabao 2-0 na kutoa picha iliyo sawa na watani wao wa jadi Yanga, ambao nao pia katika mchezo wao wa jana walichapwa mabao 2-0 na Atletico na kuwaacha mashabiki wa timu hizi mbili wakibaki na maswali mengi yasiyo na majibu.
 Mchezaji wa timu ya URA ya Uganda, Derrick Walulya (kushoto) aliyetemwa na Klabu ya Simba msimu ujao akimhadaa mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu, wakati wa mchezo wa kuwania kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA. 
Mchezaji mpya wa Simba, akiwatoka mabeki wa URA wakati wa mchezo huo leo jioni. Picha na MdauT

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...