Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 11, 2015

MABONDIA WA DAR WATAMBA KUWASAMBALATISHA WA MOROGORO


Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Kaike Siraju katikati akimwinua mkono juu bondia Thomas Mashali wakati wa utambulisho wa mpambano wake na Fransic Cheka utakaofanyika desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro kushoto ni bondia Lulu Kayage atakaezipiga na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota Kaike Siraju akimwinua mkono juu bondia Lulu Kayage wakati wa kutambulisha mpambano wake wa ubingwa na Mwanne Haji mpambano utakaofanyika Jamuhuri Mkoa wa Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA wa Dar watamba mabondia hawo wanaotarajia kupanda uringoni desema 25 mkoa wa morogoro wakiongozwa na Thomas Mashali aliye jiakikishia ushindi wa mapema kwa kumtwanga Fransic Cheka wa morogoro katika raundi za awali

mpambano wa raundi kumi utakaopigwa katika uwanja wa Jamuhuri morogoro bondia huyo mwenye mashabiki lukuki nchini aliendelea kujitamba kuwa anakwenda morogoro kufanya kazi aliyotumwa na wapenzi wa ngumi ivyo ato waangusha

kwa kuwa  wapenzi wa ngumi watakuja kuangalia mchezo nitakao mchezea ni tofauti na yote ninayochezaga dozi ya cheka ni maalumu kwake tu

nae bondia bingwa wa mikanda miwili wa WPBF na U.B.O Africa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amejigamba kumtwanga bondia Twaha Kiduku kwani bado ni kinda sana kwa ata hivyo wembe kaulilia mwenyewe asubili kukatwa tu siku hiyo

nae bondia pekee wa kike nchini anaekuja kwa kasi ya ajabu baada ya kufanya vizuri katika michezo yake ya kimataifa Lulu Kayage amejigamba kuwa atamsambalatisha vibaya Mwanne Haji kwani atofika katika raundi ya sita ambapo kwa sasa sio lulu yule wa zamani 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...