Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 14, 2018

BONDIA VICENT MBILINYI KUPAMBANA NA SAIDI KIDEDEA SEPTEMBA 15 UWANJA WA NDANI WA TAIFA

Mabondia Saidi Mpoma 'Kidedea' kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Saidi Mpoma 'Kidedea' kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu


BONDIA Vicent Mbilinyi  amesaini mkataba wa kuzipiga na Saidi Mpoma 'Kidedea' septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa

akizungumza mara baada ya kusaini mkataba uho mbilinyi amesema kuwa atafanya mazoezi ya kutosha ili aweze kushinda kwa kuwa ngumi kwake ni kazi kazi na kuwataka mashabiki wake wote kujitokeza siku hiyo kushudia mpambano uho kwani ato waangusha amejipanga vizuri


Nae Saidi Kidedea amesema anashukuru kwa kupata mpambano uho kwana yeye siku zote achaguwi mabondia kwake yoyote anaekuja mbele yake kazi anayo na amepanga kummaliza mpinzani wake katika raundi za awali ili asiwachoshe mashabiki anao wategemea

aidha ameomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kumsapoti kwani ato wahangusha ata kidogo

Na mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema siku hiyo kutakuwa na mapambano makubwa ambapo bondia Fred Sayuni atapambana na Haidari Mchango wakati George Dimoso atavaana na Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe'  na Imani Mapambano ataoneshana umwamba na Paul KamataSadiki Momba atavaana na Mohamed Kashinde na bondia machachari Tonny Rashidi atavaana na Said Zungu  Ramadhani Shauri atakumbana na  Saidi Amani

Mbali na mipambano hiyo ya ngumi siku hiyo pia kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...