Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 1, 2019

SUNDAY KIWALE 'MORO BEST' NA IBRAHIMU MAKUBI KUPIGANA MOROGORO MARCH 2 MSAMVU TERMINAL


Bondia machachali nchini Tanzania Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto kutoka Dar es Salaam Tanzania akitunishiana misuli  na mpinzani wake Said Chalachim kutoka Ifakala mabondia hawo watazipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal Pub ulipo msamvu Morogoro

Promota wa masumbwi nchini Kaike Siraju akiwainua mikono juu bondia Ibrahimu Makubi na Chales Chilala baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga march 2 katika ukumbi wa Terminal pub ulipo msamvu morogoro    
Na
Mwandishi Wetu

MABONDIA kutokwa kwa Super D Coach Uhuru GYM Sunday Kiwale  'Moro Best' na Ibrahimu Makubi wapo mkoani morogoro kwa ajili ya mpambano yanayo wakabili ambapo Sunday Kiwale 'Moro Best' atamkabili Said Chalachim kutoka Ifakara wakati Ibrahimu Makumbi atazipiga na Charles Chilala nae kutoka Ifakara

akizungumza baada ya kupima uzito kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wake wapo vitani hivyo awatofanya ajizi wala kuwa na msalia Mtume kwani kazi waliyotumwa na mashasbiki zao kutoka Dar es Salaam si yakitoto na awatotaka kuwangusha kwa kuwa wao ni watu wa kazi kazi

nae bondia kiwale anaetamba katika uzito wake amesema kuwa mabondia wengi nchini wanamuogopa ndio mana amekuja kucheza Mkoani ili kuendeleza kipaji chake kisije kikapotea bule kwa sababvu ya kuogopewa na mabondia wa Dar es salaam katika uzito wake kwani kazi yangu wanaijua na kuitambuwa niwapo ulingoni

na bondia Makubi alisema kuwa yeye ni bondia mchanga sana katika ngumi za kulipwa ila ni motto mkali katika masumbwi hivyo nawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kwa wingu kushudia kazi atakayo ifanya

Mabondia hawo wote watakuwa wakisindikiza mpambano wa ubingwa kati ya Twaha Kiduku wa Morogoro na Mada Maugo watakaozipiga raundi kumi kugombea ubingwa wa Taifa nchini

Promota wa mpambano uho kaike Siraju alieleza kwa kusema kuwa ameandaa mapambano mengi sana nchini ususani Morogoro sasa baada ya kumuibua Fransic Cheka sasa ameibuwa mabondia wengine mbalimbali kutoka moro pamoja na vitongoji vyake hivyo kazi kwao mashabiki kutoa sapoti

aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mitanange mingine ya kukata na shoka ambapo bondia Epson John atazipiga na Adamu Ngange na Cosmasi Cheka atakabiliana na Amani Bariki na kingilio katika mapambano yote hayo ni tsh 7000 na V.I.P 15000  na nyote mnakaribishwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...