Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 7, 2015

MABONDIA RAMA SHAURI NA LULU KAYAGE WAPAA AFRIKA YA KUSINI


Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwa na mabondia Lulu Kayage kulia na Ramadhani Shauri wakienda kupanda ndege kwenda afrika ya kusini mabondia hawo wanapanda uringoni agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA LULU KAYAGE

MABONDIA WAKIWA NA WADAU MBALIMBALI WA MASUMBWI KABLA YA KUPAA AFRIKA YA KUSINI KWA AJILI YA MCHEZO WAO WA AGOST 9


Bondia Lulu Kayage kulia  akihakiki nyalaka zake za kusafiria kushoto ni mshauri wake wa karibu Hamisi Berege kutoka kambi ya mchezo wa ngumi Ilala Lulu amenda Afrika ya kusini kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akingia katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa julius nyerere kwa ajili ya safari pamoja na mabondia Lulu Kayage kushoto na Ramadhani Shauri mabondia
kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mali Mpya zaingia Isere Sports

Wednesday, August 5, 2015

SUPER D AZAWADIA BONDIA LULU KAYAGE VIFAA



Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila amemzawadia bondia Lulu Kayage vifaa vya mchezo wa masumbwa baada ya bondia huyo kuchaguliwa kwenda kupigana Afrika ya kusini agust 9 mwaka uhu vifaa hivyo alivyokabidhiwa bondia huyo ni Gumshilt 'kikingiakinywa' clip bandeji pamoja na fulana yenyenembo ya Tanzania vifaa ambavyo ni lazima bondia awe navyo

Lulu kayage anaondoka nchini agous 7 kwenda afrika ya kusini kupambana na Lizbeth Sivhaga Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo siku ya jumapili

akizungumza baada ya kupokea msaada huo Lulu alimshukuru Super D kwa kujitolea alichojaliwa kwa kuwa sio watu wote wenye mioyo ya kujitolea kama yeyey hivyo amemwakikishia kumpa zawadi ya ushindi ili aendelee kuwa na furaha mana ushindi wangi ni wa watanzania wote hivyo sito wahangusha

nae Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallahh 'ostadh' aliongeza kwa kusema Lulu atambatana na bondia Ramadhani Shauri atakaekwenda kupambana na bondia mzoefu Philip Ndlovu  siku hiyo hiyo msafara huo utakuwa na watu watatu ukiongozwa na mimi mwenyewe pamoja na mabondia wawili 

ata hivyo namshukuru kocha Super D kwa kumzawadia Lulu kwani tungepata watu wengi wa kujitolea kwa moyo mmoja kama yeye michezo yetu ingefika mbali zaidi Duniani

LULU KAYAGE KUZIPIGA AFRIKA KUSINI




Bondia Lulu Kayage (kushoto) akimrushia konde bondia  Hamisi Berege wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwene Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala jijini


MABONDIA wawili wa ngumi za kulipwa wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Akizungumza jijini kocha wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila  'Super D' aliwataja mabondia hao kuwa ni Lulu Kayage na Ramadhan Shauri.

“Lulu na Shauri wamepata mapambano yatakayochezwa Agosti 9, hivyo wataondoka kesho kwa ndege ya shirika la Ethiopia “, alisema Mhamila.

Pia Mhamila alisema Lulu atapigana na Lizbeth Sivhaga na Ramadhan Shauri atapigana na bondia mzoefu Philip Ndlovu 

Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo hivyo watanzania mnawaombwa kuwaombea mabondia hao ili waweze kupeperusha bendera ya taifa vema.

MABONDIA LULU KAYAGE RAMADHANI SHAURI KUPIGANA AFRIKA KUSINI 9 Aug


FAMILIA INAPOKUTANA KWA MARA NYINGINE STAR BOY NA SUPER D

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa na kaka yake Shabani Mhamila Star Boy wa pili kulia baada ya kupotezana kwa mda




Rajabu Mhamila Super D kulia

YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTO YATIMA


Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.

Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini  changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.

Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia  jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.

Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.

"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.
Miss kilimanjaro ambassador 2015,Yolanda Shayo akiwa katika picha ya pamoja na mtoto ambae anaosha kalamu ikiwa ni sehemu ya zawadi zilizogawiwa na mrembo huyo.
 Yolanda Shayo akisaidia kugawa chakula kwa watoto na viongozi wa vituo hivyo,ambapo alishiriki kwa pamoja nao katika chakula cha mchana.

WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE

IMG_0282
Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.
Na Mwandishi wetu, Kibaha
MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.
Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.
Aliahidi ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.
Mganga huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha panapohusika.
Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.
Akitoa salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia marafiki wa Afrika.
Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.
Aliwaomba wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.
Alisema kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia wengine katika kuonesha upendo.
Aidha alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati hiyo likiwa limekamilika.
Wazo la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.
Alisema pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.
Katika risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.
Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.
Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Wamesema kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.
Zahanati hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia umeme wa sola na jenereta .
Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.
IMG_0289
Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.
IMG_0301
Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.
IMG_0323
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr. Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,
IMG_0335
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akimpa mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.
IMG_0341
Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.
IMG_0348
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi (kulia) akimkabidhi zawadi Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni. Anaye shuhudia tukio hilo ni Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju...
IMG_0351
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akikabidhi zawadi kwa wadau waliombatana na Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Muitalia, Germano Frioni.
IMG_0354
IMG_0194
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi (wa pili kulia) pamoja na Mfadhili wa ujenzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa ya kijiji cha Vikawe, Kibaha, Muitalia, Germano Frioni wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Zahanati hiyo inayosimamiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo nchini.
IMG_0230
Muonekano wa ndani ya Zahanati ya Da. Ma Africa-DMD iliyop Vikawe, Kibaha mkoa wa Pwani.
IMG_0211
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi akiangalia chumba cha dawa katika Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.
IMG_0235
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo mara baada ya kufungiliwa rasmi Zahanati hiyo nje ya moja ya chumba cha upasuaji mdogo.
IMG_0128
Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju akiendesha ibada takatifu ya misa maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Zahanati hiyo.
IMG_9973
IMG_0089
Wanakijiji wa Vikawe wakishiriki ibada maalum wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Da. Ma Africa.
IMG_0126
IMG_0086
IMG_0265
Kwaya ikitoa burudani.
IMG_0017
Wageni waalikwa na wanakijiji wakishiriki kuimba pamoja na kwaya.
IMG_0102
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_0140
Umati wa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe.
IMG_0361
Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wafadhili waliojenga Zahanati hiyo.
IMG_9898
Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakifurahia taswira za picha za mnato kutoka kwenye kamera.
IMG_0224
Jenereta la Zahanati ya Da.Ma Africa linalotumika kutoa umeme katika Zahanati hiyo.
IMG_9881
Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati ya Da.Ma Africa kabla ya kuzinduliwa rasmi.
IMG_0247
Wanakijiji wa Vikawe na wageni waalikwa wakiingia kukagua Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...