Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 5, 2015

LULU KAYAGE KUZIPIGA AFRIKA KUSINI
Bondia Lulu Kayage (kushoto) akimrushia konde bondia  Hamisi Berege wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwene Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala jijini


MABONDIA wawili wa ngumi za kulipwa wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Akizungumza jijini kocha wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila  'Super D' aliwataja mabondia hao kuwa ni Lulu Kayage na Ramadhan Shauri.

“Lulu na Shauri wamepata mapambano yatakayochezwa Agosti 9, hivyo wataondoka kesho kwa ndege ya shirika la Ethiopia “, alisema Mhamila.

Pia Mhamila alisema Lulu atapigana na Lizbeth Sivhaga na Ramadhan Shauri atapigana na bondia mzoefu Philip Ndlovu 

Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo hivyo watanzania mnawaombwa kuwaombea mabondia hao ili waweze kupeperusha bendera ya taifa vema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...