Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 20, 2015

MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAA KUPIGANA JUMAMOSI KARIAKOO UHURU WASICHANA

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Ally Mulo watapima uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi utakaofanyika katika viwanja vya basketball vilivyopo katika shule ya uhuru wasichana Kariakoo Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu ambaye pia ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema mabondia hawo watapima uzito siku ya ijumaa sdaa tatu asubui kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi agost 22

mbali na mabondia hawo mabondia wengine watakao oneshana kazi siku hiyo ni kelvin Majiba atakaepambana na Vicent Mbilinyi wakati Husein Pendeza akioneshana umwamba na Shomari Mirundi na Raymond Mbwago atazidunda na Roger Masawe na mapambano mengine mengi ya mabondia chipkizi

mabondia hawo watapima uzito katika tawi la mashabiki wa yanga bomba lililopo mtaa wa ndanda Kariakoo na mpambano wao kufanyika siku ya jumamosi kuanzia saa kumi na mwisho kabisa itakuwa saa kumi na mbili jioni ili kila mtu afurahie ngimi izo zitakazochezwa mapema na kumalizika mapema kabisa katika siku hiyo
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vileFloyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengipia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...