Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 4, 2010

TWANGA PEPETA WATANGAZA RATIBA YA EID EL FITRI


Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” inatarajiwa kufanya maonyesho maalum katika kusherehekea sikukuu ya EID EL FITRI inayotarajiwa kusherehekewa siku ya IJUMAA tarehe 10 mwezi wa huu au siku ya JUMAMOSI tarehe 11 mwezi wa huu mwaka huu wa 2010.



Siku ya IDDI MOSI Mchana kuanzia saa nane Twanga Pepeta inatarajiwa kuanza na onyesho rasmi kwa ajili ya watoto ukumbini MANGO Garden, ambapo Zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto watakaohudhuria, Usiku Twanga pepeta inatarajiwa kuwepo hapo hapo ukumbini Mango Garden onyesho likiwa rasmi kwa watu wazima mara baada ya onyesho la watoto kumalizika.



IDD PILI usiku kuanzia saa tatu Twanga Pepeta pia inataraji kupatikana ukumbini hapohapo Mango Garden. Twanga Pepeta itafanya onyesho siku ya IDD TATU katika ukumbi wa T.C.C Chang’ombe endapo siku ya IDD MOSI itakuwa siku ya IJUMAA, Ikiwa siku ya IDD MOSI itaangukia siku ya JUMAMOSI, onyesho la IDD TATU lililopangwa kufanyika siku JUMAPILI T.C.C club CHANG,OMBE halitakuwepo.



Maandalizi yote kwa ajili ya Maonyesho rasmi ya Kusherehekea sikukuu ya IDD EL FITRI yapo tayari na Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” imejiandaa vilivyo kama kawaida yao kuwapa burudani iliyo katika kiwango cha kimataifa wapenzi wake.



Twanga Pepeta katika maonyesho yote ya Sikukuu ya IDD EL fitri wanatarajiwa kutambulisha nyimbo mpya iliyotungwa na Mwimbaji wao nyota Charles Baba inayoitwa “Dunia Daraja” pia watatambulisha shoo na rapu mpya toka kwa marepa walio katika kiwango cha juu katika Muziki wa Dansi Nchini ambao ni Msafiri Said “DIOUF”, Khalid Chuma “Chokoraa” na Saulo John “Ferguson”.


\

Twanga Pepeta ambayo imesheheni wanamuziki vijana wenye vipaji vya hali ya juu ambao kwa sasa wameliteka jiji la Dar es salaam vilivyo kwa sasa, mara baada ya kujifua vya kutosha wanakuja na staili mpya ya ya mwaka huu inayoitwa Twanga.com.. nyimbo mpya…. 2010 inawezekana. Twanga inajidai vilivyo na Vipaji vya Waimbaji Saleh Kupaza, Kalala Jr, Luizer Mbutu a.k.a “Mama B”, Rogart Hegga a.k.a “Caterpillar” Khamis Amigolas, Janeth Isinika na Charles Baba.


Katika maonyesho yote Bendi ya African Stars inatarajiwa kuzidi kutambulisha kibao chake kipya kilichorekodiwa na kusambazwa katika stesheni mbalimbali za Redio kinachojulikana kwa jina Mapenzi hayana kiapo kilichotungwa na Kiongozi msaidizi Saleh Kupaza.



ASET inawapa mkono wa IDD EL FITRI wapenzi, mashabiki na watanzania wotekwa ujumla mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani salama.
http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...