Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 17, 2012

MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA CUF KILICHOFANYIKA SHABAN HAMISS MLOO MJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14-15 Julai, 2012.


 Prof.Ibrahim Lipumbu Mwenyekiti  CUF Taifa
--
Yametangazwa leo tarehe 17/07/2012,Ofisi za CUF Buguruni mbele ya waandishi wa habari.
Baraza Kuu la Uongozi Taifa la The Civic United Front (CUF- Chama Cha Wananchi) limekutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, kikao ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Prof Ibrahim Lipumba na kufanyika katika Ukumbi wa Shabani Hamisi Mloo , Dar es salaam, Tarehe 14-15 Julai, 2012. Katika kikao hicho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limepokea, limejadili na kuzifanyia maamuzi Agenda mbalimbali zilizowasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ikiwa ni pamoja na;
1. 1. Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012
2. 2. Maandalizi ya Uchaguzi mdogo Jimbo la Bububu
3. 3. Msimamo wa Chama katika mchakato wa Maoni ya Wananchi kuhusu uandikaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
4. Uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana.
5. Hali ya Kisiasa Nchini.
Baada ya Mjadala wa kina kuhusiana na agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:
Utekelezaji wa Kazi za Chama kipindi cha Oktoba 2011-juni 2012
1. Baraza Kuu limepokea Taarifa ya Kazi za Chama kwa kipindi cha Oktoba 2011 hadi 2012. Baraza limeipongeza Kamati ya Utendaji kwa Kazi ilizofanya na kusimamia kwa kipindi pamoja na changamoto za kiutendaji zinazowakabili. Baraza Kuu limetoa msisitizo kwa Chama kuendelea kujipanga .
Kuhusu Maandalizi ya Uchaguzi Bububu
1. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhia lengo la Chama kushiriki katika Uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Bububu na kuhakikisha chama kinashinda kwa sababu jimbo hilo ni ngome kubwa ya CHAMA na hasa baada ya kutathmini matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Kuhusu uimarishaji wa Chama kupitia Jumuiya ya Vijana
1. Baada ya kazi kubwa iliyofanywa na jumuiya za chama na kuonekana kuwa zinapaswa kuimarishwa zaidi, hususani jumuiya ya vijana taifa (JUVICUF), Baraza Kuu limejadili na kukubaliana kufanya mabadiliko katika nafasi mbali mbali za Uongozi ndani ya Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilisha baadhi ya wajumbe waliokuwepo awali. Viongozi walioteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ni hawa wafuatao:-

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...