Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 9, 2012

MANISPAA YA ARUSHA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA YATIMA



Na.Ashura Mohamed-Arusha

Halamshauri  ya  manispaa  ya  Arusha  imesema  kuwa  kuanzia  sasa  itaanza  rasmi  kutenga  bajeti  kwa  ajili  ya  kuwasaidia  yatima  ndani  ya  manispaa , ambapo  bajeti  hiyo pia  italenga  misaada  kwa  vituo  mbalimbali   ili  kupunguza   changamoto  mbalimbali  ambazo  zinaikabili  vituo  mbaliombali  hapa mjini

Akizungumza   katika   harambee  kwa  ajili  ya  watoto yatima  wa  kituo  cha  watoto Matonyok Children Care  kilichopo  katika  kata  ya  Olasistri  Meya  wa jiji  la  Arusha  Bw  Gaudence  Lyimo  alisema  kuwa  mpango  huo utaanza hivi karibuni   ambapo   vituo  vya  mayatima  navyo  vitahusika   kwa  kuwa  kwa  sasa  kuna  changamoto  mbalimbali ambazo zinakabili   vituo  vya  yatima.

Bw  Lyimo  alisema  kuwa  kwa  sasa  bajeti  hityo  itahakikisha  kuwa  hata  misada  mbalimbali  ambayo inatolewa    na   wafadhili  mbalimbli  inawafikia  walengwa  ambapo  yote  hayo  yatakuwepo  ndani  ya  bajeti  hiyo.

“kwa  sasa   tumepanga  kuwa  katika  kila bajeti  ya  halmashauri   yatima  nayo  wanatakiwa   kuhusishwa   kwa  kuwa  ndani  ya  vityuo  vingi  vya  mayatoma  kuna  changamoto ambazo  zinafanya  baadhi  ya  mayatima  kushindwa  kufikia  malengo  yao”alisema  Bw  Lyimo

Pia  aliongeza  kuwa  mpango  huo  wa  kuwapa  yatima  ufadhili mbalimbali kupitia  halmashauri  hiyo pia wataweka  mpango  maalumu  wa kuhakikisha  kuwa wanawafuatilia  baadhi  ya vituo  ambavyo  vinatumia  vibaya  ufadhili  pamoja  na  jina  la yatima.

Hata hivyo  harambee  hiyo  ambayo  iliandaliwa   na  diwani  wa   kata  hiyo  Bi  Rehema  Mohamed  yatima  walifanikiwa  kupata  million  mbili , na  laki  moja  ambapo  fedha  hizo  zitatumika  kwa matumizi  mbalimbali  ya  Yatima  hao

Bi  Rehema  alieleza  kuwa   ni  vema  kama kila  jamii ihakikishe  kuwa  inawalinda  na  kuwathamani  mayatima  na  badala yake  kuwapa haki  zao  za  msingi  kwa  kuwa  kwa  sasa  ndani  ya  vituo  vingi  kuna  changamoto  ikiwemo  suala  zima  la  ukame


Alimalizia  kwa  kusema  kuwa  kutokana na  changamoto  ambazo  zimo kwenye  vituo  wengi  wa  mayatima  wanakosa  haki zao  za  msingi  jambo  ambalo  linawafanya  waweze  kukimbia  katika  vituo  vyao  ambavyo  wanalelewa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...