.
Hapa Mkurugenzi akitoa amri umeme ukatwe maramoja. |
WIZIZI wa umeme kwa njia ya mtandao umemfanya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Injinia William Mhando, kuingia mitaani kushiriki zoezi la ukaguzi wa mita za wateja.
Akiwa kwenye zoezi hilo ambalo kwa wananchi lilionekana si la kawaida kutokana na kufuatana na baadhi ya mameneja na wataalamu Mhando alisema wamepokea taarifa ambazo si nzuri za wizi wa umeme kwa njia ya mtandao hali iliyomlazimu kufuatilia kwa makini tangu ngazi ya chini kabisa.
Mhando alisema tangu kuanza kuzifanyia kazi taarifa hizo wamekamata watu 2 Dodoma na 3 Dar es Salaam ambao kesi zao zimefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutumia umeme ambao haujulikani umenunuliwa wapi.
“Utakuta mteja amenunua umeme wa Sh10’000/ kwetu lakini unapokwenda kukagua utakuta anaumeme wa zaidi ya pesa hizo, nah ii inamaanisha kuna sehemu zingine wananunua tofauti na Tanesco ambapo kwenye mfumo haupo,” Alifafanua Mhando.
Alipoulizwa kuhusu sababu za kuwepo kwa tatizo hilo Mhando alisema tuna wasiwasi kuwa mtaalamu aliyekuja kuingiza mfumo huo aliacha program mtaani na kufanya watu wenye nia mbaya kutumia nafasi hiyo.
Hata hivyo Mhando alisema tatizo hilo limegundulika haraka kutokana na mita maalum (Automatic Meter Reader) zilizofungwa ambazo husomwa moja kwa moja kwenye Tanesco bila ya kwenda kwa mteja na ndio maana tatizo hilo limegundulika haraka.
No comments:
Post a Comment