Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 12, 2012

MIKOA MITANO YAKAMILISHA MASHINDANO YA SAFARI POOL TAIFA NGAZI YA MKOA


  Bingwa wa mchezo wa pool mmoja mmoja (Singles) Mkoa wa Shinyanga, Ndala Ndefu akionyesha kitita chake cha Shilingi laki tatu na nusu mara baada ya kutwaa ubingwa wakati wa mashindano Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa  yaliyofanyika katika Klabu ya Garden mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa mchezo wa pool mmoja mmoja(singles) Mkoa wa Shinyanga, Ndala Ndefu akicheza dhidi ya mpinzani wake Majaliwa Cyipilian wakati wa mashindano Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa  yaliyofanyika katika Klabu ya Garden mwishoni mwa wiki.
Na Michael Machellah;
MIKOA mitano kati ya 16 inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mikoa imekamilisha fainali za ke mwishoni mwa wiki hii kwa kupata klabu,mchezaji mmoja mmoja (single) wa kiume na kike.
Katika mashindano hayo yalihudhuriwa na wageni rasmi mabalimbali kila Mkoa ambao pia waligawa zawadi kwa washindi.Mshindi wa kwanza alijinyakulia Shilingi laki saba, mshindi wa kwanza wa kiume alipata shilingi laki tatu nusu na wa kike laki mbili na nusu pamoja na zawadi zingine kwa washindi wa pili na tatu.
Mkoa wa Shinyanga mabingwa ni Klabu ya New Stand, mchezaji wa single wanaume ni Ndala Ndefu na singles wanawake ni Sada Tuwa, Mkoa wa Kagera mshindi wa timu ni klabu ya Balele,singles wanaume ni  Hakimu Mzamili na singels wanawake ni Angel Mfaume
Tabora mabingwa ni Klabu ya Texas, singles wanaume ni Waziri Ally na singles wanawake ni Angel Mfaume wakati Manyara mabingwa ni Klabu ya Janja Wild, singles wanaume ni Ally Nada na singles wanawake ni Chiku Mohamed.
Kilimanjaro mabingwa ni klabu ya Mbosho,singles wanaume ni Teter George na singles wanawake ni Cecilia Kileo.
Washindi hawa watawakilisha mikoa yao katika mashindano ya Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Semptemba jijini Mwanza kwa kushilikisha Mikoa 16 ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...