Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 16, 2012

MWANDISHI MWANDAMIZI WA MICHEZO AFARIKI DUNIA


Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo, Chris Mwambonda amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Marehemu Mwambonda, Mawazo Lusonzo,  mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na mipango ya maziko inafanyika nyumbani kwa mama yake mzazi Goba na mipango ya mazishi inafanyika huko huko, taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Pichani ni moja katika ya matukio aliyoshiriki enzi za uhai wake ambapo hapa anaonekana akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo yaliyowashirikisha wahariri wa michezo na Mkurugenzi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leonard Thadeo baada ya semina ya wahariri wa michezo iliyofanyika Juni 10 2010.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...