Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 10, 2012

NASSARI AIPONGEZA HALMASHAURI YA MERU KUPATA HATI SAFI
Na.Ashura Mohamed-ArumeruMbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Bw.Joshua Nassari ameipongeza halmashauri ya Meru kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada ya halmashauri hiyo kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za umma.
Akizungumza katika baraza la madiwani la lililofanyika katika halmashauri hiyo bw.Nassari alisema kuwa halmashauri nyingi zinashindwa kusimamia matumizi bora ya fedha halia ambayo inapelekea hamlashauri hizo kupata hatia chafu ama za mashaka.

Bw.Nassari alieleza kuwa ili kuhakikisha kuwa halmashauri hiyo iweze kuendelea kufanya vizuri ni wazi kuwa ushirikiano wa karibu wa viongozi hao unahitajika bila kujali  itikadi za vyama vya siasa ili wananchi wa jimbo hilo waweze kupata maendeleo.

Aidha alisema kuwa pindi halmashauri inapopata hati chafu serikali kupiti Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) hupunguza fedha za miradi ya maendeleo ama kutopeleka kabisa kutokana na kuona kuwa kama halmashauri hizo hazina mahitaji ya fedha kutokana na matumizi mabaya hali ambayo inapelekea miradi ya maendeleo kurudi nyuma.

Pia alieleza kuwa swala la fedha  ni tatizo katika halmashauri nyingi hivyo ni vyema kama kuhakikisha kuwa halmashauri inakuwa na mipango madhubuti na mikakati ili miradi mbalimbali ya maendeleo isirudi nyuma wala kuyumba.

Lakini hata hivyo bw.Nassari alieleza wazi kero ya gari la Zimamoto katika halmashauri ya Meru ni kubwa lakini jitihada za makusudi zinahitajika ili kwa kushirikiana na halmashauri hiyo ili gari liweze kupatikana ili kupunguza madhara pindi ajali za moto zinapojitokeza.

Halmashauri ya Meru ni moja kati ya halmashauri zilizopatiwa hati safi pamoja na kuongoza katika nafasi ya kwanza kitaifa kwa upande wa Usafi sherehe zilizofanyika mkoani Kilimanjaro na Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...