Na Ashura Mohamed-Arusha
KOCHA
mkuu
wa timu ya Tanzania(Taifa Stars),Kim Poulsen anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi
kwenye mashindano ya ligi ya ya kuibua vipaji vya soka la vijana
inayojulikana kama Moivaro Youth Football League(MYFL) ambayo itatimua
vumbi mnamo septemba 29 mwaka huu mkoani Arusha.
Pia,viongozi
mbalimbali wa ngazi za soka mkoani Arusha na nchini kwa ujumla akiwemo mtaalamu
wa masuala ya ufundi wa shirikisho la soka nchini(TFF),Sunday Kayuni
anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika ligi hiyo.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi na mwasisi wa Taasisi ya Future Stars
Aademy ya jijini hapa,Alfred Itaeli alisema kwamba ligi hiyo itashirikisha timu
za wanawake pia ambapo usajili wa timzu zitakazoshiriki unataraji kuanza Agosti 18 mwaka huu.
Itaeli ,alisema
kwamba kabla ya ligi hiyo kutimua vumbi
wameandaa mafunzo ya wiki mbili kwa waamuzi wenye umri
kati ya miaka 8 hadi 15 ambao watatumika kuchezesha ligi hiyo ili
kuepuka gharama za kukodi waamuzi mbalimbali ambapo mafunzo hayo yatandeshwa na
mwamuzi mkongwe nchini Billy Mwilima.
Alitaja
lengo kuu la ligi hiyo ni kukuza vipaji vya soka nchini na kuweka ushindani kwa
kila rika huku akisisitiza kuwa kwa kuwa ligi hiyo haina wadhamini wameamua
kutoza kiasi cha sh,100,000 kama ada za kiingilio.
No comments:
Post a Comment