Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 9, 2012

PROFESA LIPUMBA AITAKA SERIKALI KUZINGATIA HOJA ZA WAISILAMU KUHUSU KATIBA MPYA




Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kuzingatia hoja mbalimbali za waislamu katika mchakato wa katiba mpya ili kumaliza zoezi hili kwa wakati.

Amesema kutokana na kutosikilizwa kwa waislamu kuhusu hoja zao dhidi ya uundwaji wa katiba mpya ni kikwazo cha utekelezaji wa zoezi hilo linalotarajiwa kufikia tamati Aprili 26 mwaka 2014.

Profesa Lipumba alikuwa akihutubia Kongamano la Waislamu jijini hapa lililoandaliwa na Jukwaa la Katiba Mkoa wa Arusha juzi na kuhadharisha kuwa iwapo hoja hizo hazitazingatiwa itakuwa vigumu kukamilika kwake.

“Mchakato wa Katiba Mpya sasa ni miezi 16 na iunatarajiwa kukamilika Aprili 26 mwaka 2014, ni wazi iwapo zoezi litaendelea kukumbwa na malalamiko kama haya ya waislamu itakuwa vigumu kukamilika kwa wakati, na iwapo litakamilika basi hiyo haitakuwa katiba iliyokamilika kwakuwa haitoshelezi mawazp na maoni ya wananchi”
Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanajitosa katika mchakato wa kutoa maoni bila kukosa ikibidi kwa kurikodi kile wanachokipendekeza ili katiba hiyo itakapokamilika waione iwapo inayo maoni waliyotoa ama maoni hao hayapo waikatae.

Alisema mchakato wa kudia kuwepo kwa katiba mpya kulianza miaka ya tisini kupitia chama chake, na hata mwaka 2001 walivamiwa na Polisi wakiwa katika maandamano ya amani wakidai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ambapo alivunjwa mkono na kuporwa saa yake na Polisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...