Erasto T. Ching’oro – Kitengo cha Mwasiliano, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto
Waziri wa Maendeleo ya Jaimii na Jinsia na watoto Mheshimiwa Sophia M. Simba (Mb.) amepongeza Mradi wa Shirika la kimarekani la Buffalo Tanzania unaolenga kutoa huduma ya elimu, afya, teknolojia na ujasiriamali kwa wasichana na wananchi wa kijiji cha Kitenga sehemu ambayo awali ilikuwa ilikumbwa na mizozo ya kikabila katika wilayani Rorya mkoni Mara.
Kiongozi wa shirika la ‘Buffalo Tanzania Education Programme’ lenye makao yake jijini Buffalo, New York, Marekani Bibi Katie Biggie na Dkta. Jim Hoot wameeleza mipango ya shirika hilo kwa ni kuanzisha mradi mkubwa wa huduma za elimu kwa watoto wa kike, afya, ujasiriamali na teknolojia sahihi kwa kijiji cha Kitenga wilayani Rorya mkoa Mara. Lengo la mpango shirika ni kuwajengea wananchi uwezo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe. Katie Biggie alimweleza Waziri Sofia M. Simba (Mb.) kwamba ujumbe wake wenye watu 12 wanawakilisha asasi mbalimbali za kiraia ambazo zina nia thabiti ya kuwekeza aktika maeneo hayo manne ili kuendeleza eneo la Kitenga, Rorya. Waratibu wa mradi huo wanatoka mji wa Buffalo katika Chuo Kikuu cha ‘Buffalo University’ na ‘State University’ jijini New York, Marekani. Ujumbe wa Buffallo Tanzania ulifika ofisini kwa waziri Sofia Simba kwa lengo la kutambulisha mradi huo unaolenga kubadilisha eneo la mzozo wa makabila ya Rorya na Tarime kuwa kituo cha elimu kwa watoto wa kike na jamii yote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment