Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 14, 2012

TPBO YATANGAZA SAFU YAKE NA KUMPONGEZA SUPER D BOXING COACH KWA JUHUDI ZA KUINUA MASUMBWI NCHINI






AWALI YA YOTE NINAMPONGEZA SANA SUPER 'D' SUPER COACH KWA JINSI ANAVYOJITOLEA KUTOWA ELIMU KWA NJIA YA DVD ZA MASUMBWI ,ILI WATU WAUJUWE VILIVYO MCHEZO WA NGUMI ZA AINA ZOTE [RIDHAA NA KULIPWA ].MIMI BINAFSI NIKO TAYARI KUTOWA USHIRIKIANO WANGU KUPITIA MTANDAO WAKE ILI HATA WALE WAANDISHI AMBAO HAWANA UPEO WA KUANDIKA KUHUSU MCHEZO WA NGUMI KWA UJUMLA WAKE NAO TUHAKIKISHE WANAIPATA TAALUMA HII YA KUANDIKIA NGUMI KIJUMLA, WAPO BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO AMBAO MCHEZO WA NGUMI UNAWAPA TAABU SANA JINSI YA KUUANDIKIA.

HATA INAPOTOKEA UBISHANI WA KISHERIA KTK NGUMI ZA KULIPWA ,WAO HUANDIKA KAMA NI MIGOGORO WAKATI SIYO MIGOGORO ;-



NINAWAONMBA SANA NDG WAANDISHI WAITUMIE  MTANDAO WA http://superdboxingcoach.blogspot.com/  KWA KUTUULIZA MASWALI JUU YA SHERIA  NA TARATIBU ZA NGUMI ZA KULIPWA WAKATI WOWOTE WANAPOHITAJI KUJUWA ,KWANI KUULIZA SIYO UJINGA,NA MWANADAMU HAKAMILIKI HAWEZI KUJUWA KILA KITU .

MIMI NITAJITAHIDI SANA KUWATAFUTIA MAJIBU SAHIHI KWA MASWALI AMBAYO MTAPENDA KUYAJUWA MAJIBU YAKE, INSHAALLAH

NINAAMUWA HIVI KWA SABABU NINAWAPENDA SANA SANA WAANDISHI WOTE WA HABARI ZA MICHEZO KAMA MIMI MWENYEWE NINAVYOIPENDA NAFSI YANGU .

KWA HIYO NISINGEPENDELEA TAALUMA YENU IINGIZWE KTK MALUMBANO KWA AJILI YA MAMBO AMBAYO YANAHITAJI TAFSIRI ZA KISHERIA .

NINAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWAMBA KWA KIASI KIKUBWA NINAO UFAHAMU WA MAMBO HAYA NA SITAKUWA MCHOYO KUKUPENI ILI MUYAWEKE NDANI YA MADAFTARI YENU KAMA NI ELIMU RASMI .

INGEFAA SANA KAMA TUNGEFANYA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO LKN KAMA MJUAVYO VYOMBO VYENU NDIYO WADHAMINI WETU WAKUBWA KWA KUTUSAIDIA KUUTANGAZA MCHEZO WA NGUMI NA HATUNA WADHAMINI WA KUTUWEZESHA KWA PESA.

WAPO BAADHI YA WAANDISHI AMBAO MPAKA LEO WANAAMINI ETI TPBO NI MTU MMOJA AITWAYE YASSIN ABDALLAH-USTAADH HIVYO HAKUNA VIONGOZI WENGINE NDANI YA TPBO.

NINGEPENDA WAJUWE KWAMBA HATA MWILI WA BINAADAMU UNA VIUNGO VINGI SANA ,NA VIKO VIUNGO MUHIMU KTK MWILI WA BINAADAMU AMBAVYO VIKIKATIKA TU ,BASI BINAADAMU ANAKUFA NACHO NI KICHWA ,KICHWA KIKIONDOLEWA TU NA UHAI WA BINAADAMU UNATOWEKA .USTAADH NI KICHWA TU.

NI VYEMA KWA KUTUMIA BLOG YAKO WAANDISHI WOTE WAUJUWE UONGOZI WA TPBO;-

[1]  RAIS  NA MSEMAJI MKUU ;-YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH

[2] KATIBU MKUU ;-IBRAHIMU KAMWE [BIGRIGHT]

[3]KATIBU MSAIDIZI  PIA MWAMUZI ;-SAIDI CHAKU

[4] MKURUGENZI MKUU WA UFUNDI NA UTAWALA PIA JAJI;- FIDEL HYNES

 [5] [MSHAURI WA RAIS ;-BENJAMIN CHUMA

[6] MWAMUZI MKUU ;-SAKWE MTULYA

 [7] MWENYEKITI WA KAMATI YA WAAMUZI - NDG PONELA [MOROGORO]

[8] MWAMUZI -KONDO NASSORO

NAFASI YA MAKAMU WA RAIS ;- IKO WAZI BAADA YA DOCTOR SYSTUS LISSA KUWA NJE YA NCHI KWA MUDA MREFU , ANATAFUTWA MWINGINE NA AJITOKEZE ANAYEPENDA KWA MASHARTI YA -ELIMU YA CHUO KIKUU NA AWE JASIRI, ASIYEOGOPA KUSEMA UKWELI HATA IKIBIDI KUHATARISHA MAISHA YAKE , NA ATAMBUWE WAZI KWAMBA ATAJILIPA KWA JUHUDI ZAKE ZA KUHAKIKISHA MAPAMBANO MENGI ANAYALETA NDANI YA TPBO .

IMEANDIKWA NAMI;-

YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS-TPBO MAWASILIANO ZAIDI  0713644974

HIYO NDIYO SAFU YA UONGOZI WA TPBO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...