Mkurugenzi
wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako (katikati) akiongea na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha
fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga kupitia kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke
wa Tanzania” siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza
uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi Mtendaji wa
kampuni ya Montage Teddy Mapunda, kulia ni Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
M, Jacqueline Woiso.
Makamu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso (kulia) akisisitiza jamii
nzima juu ya kutambua umuhimu wa kuwasomesha wakunga nchini ambapo azma hiyo
itafanikiwa kwa kuunga mkono kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa
Tanzania”. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.
Mkurgenzi
Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy Mapunda (kushoto) akiwashukuru washirika
wanaoendelea kuunga mkono kameni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”,
baadhi ya washirika hao ni ITV/Radio One, Clouds Media Group, Banki Kuu
Tanzania (BOT), Serena hoteli, benki ya NBC, Toyota Tanzania Tanzania One,
DSTV, PPF, TACAIDSWHO na MSD. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania
Dkt. Festus Ilako.
No comments:
Post a Comment