Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 5, 2013

KINANA ATOA MSAADA WA TREKTA KWA VIJANA MKOA WA NJOMBE, ATEMBELEA CHUO CHA VETA MAKETE


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilima shamba kwa kutumia Trekta muda mfupi kabla ya kukabidhi trekta hilo lenye tahamani ya sh. mil. 42, kusaidia miradi kilimo ya vijana mkoani Njombe. Hafla hiyo ilifanyika katika shamba la vijana la heka 500 katika Tarafa ya Ikuwo, wilayani Makete leo.
Kinana yupo katika ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilanai ya Uchaguzi ya CCM.
 Kinana akishuka kwenye Trekta baada ya kulima katiak hafla ya kukabidhi msaada huo wa Trekta kwa vijana wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kusaidia  kilimo.Anayetangaza kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Kinana akimkabidhi ufunguo Mwenyekiti wa Vijana 252 wa Tarafa ya Ikuwo, wilayani Makete, ikiwa ni ishara ya kukabidhi msaada Trekta uliotolewa na CCM kwa vijana wa Mkoa wa Njombe
Kijana aliyevaa kofia aina ya mzula wenye rangi za bendera ya Chadema, akiwa miongoni mwa vijana 252  wa mradi wa kilimo wa Kata ya Ikuwo, walipokuwa wakikabidhiwa msaada wa Trekta uliotolewa na CCM kwa vijana mkoani Njombe.
 Kinana akiuhutubia baada ya kukabidhi Trekta kwa ajili ya kilimo kwa vijana, ambapo alisema msaada huo uliotolewa na CCM utawasaidia vijana wote mkoani Njombe bila kujali itikadi za vyama.
 Katibu wa NEC-CCM wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe, baada ya msafara wa Kinana kuwasili wakitokea Mkoa wa Mbeya baada ya kumaliza ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo.
 Kinana (kushoto) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kulia) na kukaribishwa Mkoa wa Njombe na Aseri Msangi (katikati)
Kinana na Nape wakiongozwa na Chipukizi walipoingia wilaya ya Makete kuanza ziara katika Mkoa wa Njombe.


 Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumlaki eneo la Mfumbi, akitokea katika ziara mkoani Mbeya.
Dk. Migiro akisalimia wananchi wa katika hafla ya Kinana kukabidhi Trekta kwa vijana Mkoani Njombe leo.

 Kinana akiungana na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la wawanji katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mlengo, Ikuwo, wilayani Makete.
 Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mlengu, Tarafa ya Ikuwo wakiwa na hamu ya kumona Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mlengu, Kata ya Ikuwo, Makete.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akijaribu moja ya vyerehani katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Makete, wakati Kinana alipotembelea chuo hicho.
 Kinana  (kulia) akiangalia moja ya mashine ya kuranda mbao katika darasa la uselemala katika chuo hicho cha VETA
 Kinana akinyunyizia maji kwenye mti aliopanda katika chuo hicho.
 Nape akinyunyizia maji kwenye mti alioupanda katika chuo hicho
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM na viongozi pamoja na walimu wa chuo hicho cha VETA. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...