Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, December 29, 2013

TAN COMMUNICATION MEDIA YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU



DSCF1967Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akimkabidhi Mlezi mkuu wa kituo cha Moshono Fundation msaada katika kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo jijini Arusha juzi tarehe 26/1213 katika viwanja vya Matongee  Carnivo.
DSCF1941
KAMPUNI ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa chakula cha pamoja  cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao jamii ya watanzania imewasahau.
Mwakoyo alisema kuwa  watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa  na kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke na wameachwa peke yao.
“Watoto wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
Aidha aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji ya chakula kila siku.
“Naomba niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
Tukio hilo liliofanyika katika viwanja  vya  Matongee  Carnivo  limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
Vituo hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara na Karama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...